Loading...

Tetemeko la ardhi laua watu zaidi ya 100 nchini Iran na Iraq

Tetemeko la ardhi nchini Iran na Iraq lasababisha vifo vya watu zaidi ya 100
Tetemeko la ukubwa wa 7.3 katika vipimo vya richa limekumba eneo la kaskazini mwa Iran na Iraq na kuua watu kadha.

Takriban watu 129 waliuawa katika mkoa ulio magharibi mwa Iran wa Kermanshah, kwa mujibu wa maafisa.

Tetemeko hilo lilizua hofu hadi kusababisha watu kukimbia kutoka manyumbani mwao kwenda barabarani.

Misikiti kwenye mji mkuu wa Iraq Baghdad, imekuwa ikifanya maombi kwa kutumia vipasa sauti.

Wengi wa waathiriwa walikuwa ni kwenye mji wa Sarpol-e Zahab, kilomita 15 kutoka mpakani.

Kulingana na kituo cha Marekani USGS tetekemo hilo lilitokea umbali wa kilomita 33.9 chini ya ardhi la lilisikika nchini Uturuki, Israel na Kuwait.

Uharibifu umeripotiwa kuetka katika vijiji vinane kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Iran Morteza Salim.

Baadhi ya vijiji vimekumbwa na matatizo ya nguvu za umeme na mawasiliano yamevurugwa, huku makundi ya uokoaji yakitatizwa na maporomoko ya ardhi.

Tetemeko hilo lilitokea kilimita 30 kusini magharibi mwa mji wa Halabja karibu na mpaka wa Iran kwa umbali wa kilomita 33.9 na lilisikika pia nchini Uturuki, Israel na Kuwait.
Tetemeko la ardhi laua watu zaidi ya 100 nchini Iran na Iraq Tetemeko la ardhi laua watu zaidi ya 100 nchini Iran na Iraq Reviewed by Zero Degree on 11/13/2017 09:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.