Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 23 Novemba, 2017
Harry Kane na Dele Alli (Tottenham) |
Wachezaji wa klabu ya Totenham, Harry Kane na Dele Alli wako kwenye orodha ya wachezaji watano wanaowindwa na rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez.
Yaya Toure anasema Pep Guardiola aliwafokea wachezaji wa Manchester City katika chumba cha kubadilishia nguo akidai kwamba walikuwa wavivu sana katika mechi yao dhidi ya Feyenoord walipoibuka na ushindi wa goli 1-0.
Ashley Williams anadai wachezaji wa Wales wanamshtuko mkubwa kufuatia Chris Coleman kwenda kuinoa klabu ya Sunderland, na wamekasirishwa na shirikisho la soka la nchi hiyo kuamua kumwachia kocha huyo.
klabu za Liverpool na Tottenham zinamfuatilia kwa ukaribu beki wa klabu ya Stevenage, Ben Wilmot, ambaye ameonyesha kiwango cha kuvutia msimu huu.
Nyota wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon hawezi kuondoka kutokana na mstakabali wa mkataba wake na klabu hiyo ya Uingereza. (Daily Mail)
Giovanni van Bronckhorst |
Arsene Wenger anataka aliyekuwa nyota wa Arsena na meneja wa sasa wa Feyenoord, Giovanni van Bronckhorst achukue nafasi yake atakapoondoka Arsenal.
Everton wana lengo la kumwajiri mkurugenzi wa michezo wa klabu ya RB Leipzig kama kocha wao mpya baada ya kukata tamaa kwa Marco Silva.
Zinedine Zidane anataka klabu ya Real Madrid imsajili Antoine Griezmann kutoka kwa mahasimu wao, Atletico Madrid aje kurithi nafasi ya Cristiano Ronaldo.
Manchester United wako mstari wa mbele kwenye vita ya kuwania saini ya nyota wa Bordeaux, Malcom. (Star)
Lionel Messi hatakubali kuhimia Manchester City kwa sababu ya uhusiano wake mbaya na Pep Guardiola.
Liverpool watajaribu kumsajili kiungo wa klabu ya PSG, Javier Pastore mwezi Januari.(Express)
Arsenal iko kwenye mazungumzo na klabu ya PSG juu ya uhamisho wa mkopo wa nyota wao, Julian Draxler.
Wawakilishi wa Diego Simeone wamekutana na klabu ya Everton kuelezea mapenzi aliyonayo juu ya nafasi ya kazi ya umeneja iliyowazi.
Joao Mario |
Klabu ya Inter Milan iko tayari kumuuza Joao Mario kwa paundi milioni 26 ikiwa ni miezi kumi na nane tu imepita baada ya kumsajili nyota huyo kwa paundi milioni 40. (Sun)
Matumaini ya klabu ya West Brom kumshawishi Sam Allardyce awe meneja wao yamezidi kufifia huku Gary Megson akijiandaa kukiongoza kikosi hicho kuivaa Tottenham siku ya Jumamosi.
Klabu ya PSG inatarajiwa kuingia katika vita kubwa na Manchester City kuwania saini ya Alexis Sanchez mwezi Januari.
Meneja mpya wa Leicester, Claude Puel anatarajia kuanza kukifanyia mabadiliko kikosi chake, na ana nia ya kuwauza Ahmed Musa, Leonardo Ulloa na Yohan Benalouane ifikapo mwezi Januari. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamis Tarehe 23 Novemba, 2017
Reviewed by Zero Degree
on
11/23/2017 03:12:00 PM
Rating: