Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 17 Novemba, 2017

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo
Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid ya Uhispania, Cristiano Ronaldo amesema hana wasiwasi yoyote ya kukutana na PSG ya Neymar kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Pep Guardiola ameleta umoja kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha klabu ya Manchester City kwa kupiga vita matumizi ya 'SmartPhone' na kuzuia mitoko ya wachezaji wake.

Chris Coleman
Sunderland wamegeukia kwa Chris Coleman baada ya kushindwa kumshawishi  Michael O'Neill. (Daily Mail)

Luis Suarez anaweza kutishia kuondoka Barcelona endapo mpango wa klabu hiyo kumsajili Antoine Griezmann utafanikiwa. 

Barcelona wanahisi Mesut Ozil hatakuwa na gharama kubwa zaidi Phillipe Coutinho endapo watajaribu kumsajili mwezi Januari (90min)

Manchester United wanaimani Jose Mourinho hataondoka Old Traford katika majira ya joto mwakani. (Guardian)

Manchester United wanatarajia kumpa Jose Mourinho ofa ya mkataba wenye maslahi ya kumfanya aipotezee PSG.

Virgil van Dijk 
Klabu ya Southampton inahitaji paundi milioni 70 ili kumwachia Virgil van Dijk baada ya meneja wao, Mauricio Pellegrino kukiri kwamba ni vigumu kubakiza nyota huyo kikosini msimu ujao.

Meneja wa Leicester, Claude Puel anataka kumsajili Hatem Ben Arfa ifikapo mwezi Januari. (Mirror)

Mmiliki msaidizi wa klabu ya Swansea, Steve Kaplan ameuunga mkono jitihada za meneja wa klabu hiyo, Paul Clement.

Meneja wa Timu ya Taifa ya Wales, Chris Coleman anaweza kujumuishwa kwenye orodha ya mameneja wanaowaniwa na Sunderland ikiwa hatima ya kibarua itaendelea kuwa shakani. (Star)

Jose Mourinho hataondoka Manchester United na kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain.

Pierre-Emerick Aubameyang
Pierre-Emerick Aubameyang hatarini kuondoka Borussia Dortmund kufuatia kuachwa nje ya kikosi cha timu yake kwa sababu za utovu wa nidhamu.

Manchester United watarejesha mipango yao ya kuwania saini ya beki wa klabu ya Tottenham, Danny Rose ifikapo mwezi Januari.

Klabu za Everton na AC Milan zinatarajiwa kuingia kwenye ushindani mkubwa kuwania saini ya beki wa Dynamo Kiev, Domagoj Vida.

Emmanuel Adebayor anasema familia yake ilimpa presha kubwa iliyokaribia kumfanya afikirie kujinyonga. (Sun)

Jose Mourinho anafanya mpango wa kumsajili beki wa klabu ya Chelsea David Luiz na yuko tayari kujaribu mbinu zake ifikapo mwezi Januari.

Kazi ya David Unsworth kama meneja wa muda wa klabu ya Everton haioneshi kupata ukomo kufuatia vikwazo vinavyoikumba klabu hiyo kwenye mchakato wa kutafuta meneja wa kudumu kukinoa kikosi hicho.

William Carvalho
Sporting Lisbon wameiambia klabu ya West Ham kuwa wako tayari kutoa ofa ya paundi milioni 28 kwa ajili ya William Carvalho mwezi Januari. (Express)

Gharama za ujenzi wa Uwanja mpya wa Klabu ya Chelsea zimeongezeka na kuwa zaidi ya paundi bilioni 1, mara mbili ya makadirio ya awali na kuufanya kuwa ghali zaidi barani Ulaya. (Times)

Manchester United wanaamini Jose Mourinho ana njaa ya kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na klabu hiyo, hivyo sio rahisi kuondoka mwisho wa msimu huu.

Klabu ya West Brom inatarajiwa kujaribu kumsajili beki wa Burnley, Ben Mee endapo itashindwa kumbakisha Jonny Evans mwezi Januari. (Telegraph)

Tommy Wright
Brendan Rodgers anasema kuwa meneja wa klabu ya St Johnstone, Tommy Wright anaweza kuwa chaguo sahihi ama kwa Timu ya Taifa ya Ireland au kwa klabu ya Rangers.

Pedro Caixinha hatarajiwi kukaa bila kibarua kwa muda mrefu sana baada ya kuondoka Rangers kufuatia tetesi zinazodai kwamba yuko mbioni kuwa meneja wa Cruz Azul ya Mexico.

Niall McGinn anatarajiwa kurejea Aberdeen baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Gwangju ya Korea kusini. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 17 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 17 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/17/2017 12:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.