Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 4 Novemba, 2017

Danny Drinkwater akikabiliana na Bakayoko mazoezini
Viungo wa zamani wa klabu ya Leicester, Danny Drinkwater na N'Golo Kante, ambao wote kwa sasa wanaitumikia Chelsea wanaweza kuungana tena kwa mara ya kwanza kucheza pamoja dhidi ya Manchester United. (Guardian)

Arsenal walikataa kumsajili nyota wa Manchester City, David Silva mwaka 2005 kwa sababu walihofia muonekano wake.

Viongozi wa klabu wameanza kufanya mipango ya kuwazuia mawakala kuchukua pesa za usajili nje ya zile zitokanazo na mchezo kufuatia rekodi za dirisha la usajili lililopita.

Mkufunzi wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Gareth Southgate
Meneja wa Uingereza, Gareth Southgate atahudhuria katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Stoke City na Leicester kuwachunguza Jack Butland and Harry Maguire. (Daily Mail)

Karibu nusu ya klabu zote za Ligi Kuu ya Uingereza zimehojiwa na idara ya HMRC ya usimamizi wa kodi kuhusiana na usajili wa mamilioni ya paundi.

llkay Gundogan anasema kwamba, Manchester City wanakuwa kama Barcelona chini ya Pep Guardiola. (Sun)

Arsene Wenger anasema Alexis Sanchez yuko katika hali nzuri kuelekea mchezo wa Arsenal dhidi ya Manchester City siku ya Jumapili.

Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich
Roman Abramovich ametembelea kambi ya mazoezi ya Chelsea kufuatia kuenea kwa tetesi zinazodai Conte hana maelewano mazuri na wachezaji. (Mirror)

Meneja wa Bournemouth, Eddie Howe amekiri kuumizwa na jinsi Matt Ritchie anavyong'ara akiwa na jezi ya Newcastle. (Star)

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte amesema hawezi kuwa na urafiki na meneja yeyote wa Ligi Kuu. (Telegraph)

Dejan Lovren
Meneja wa West Ham, Slaven Bilic amelaani vitendo vya kumtishia kifo beki wa Liverpool, Dejan Lovren.

Graeme Murty amesema kwamba, hakuna mtu yeyote kwa kutumia akili yake timamu anaweza kuiacha kazi ya umeneja Rangers. (Express)

Pep Guardiola amedai ongezeko la mazoezi ya ziada limechangia kumweka Raheem Sterling tayari kuifungia Manchester City magoli. (Independent)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 4 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 4 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/04/2017 09:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.