Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 11 Novemba, 2017

Kiungo wa Klabu ya Chelsea, Tiemoue Bakayoko 
Chelsea wamepata pigo jingine baada ya Tiemoue Bakayoko kuumia wakati wa mazoezi.

Barcelona wana mpango wa kumpa mkataba mpya Sergi Roberto, ambaye anawindwa na Manchester City.

Gabriel Jesus amezungumzia jinsi alivyokuwa akicheza soka ndani ya gereza katika makuzi yake nchini Brazil.

Hector Bellerin
Klabu ya Juventus imeripotiwa kufanya mazungumzo na wawakilishi wa nyota wa Arsenal, Hector Bellerin juu ya uhamisho wa kushtukiza.

Manchester United wako kwenye majaribio ya kumnasa kinda anayeibukia mwenye asili ya Argentina, Enzo Diaz. (Sun)

Paul Pogba anasema kwamba, nyota wa Manchester United, Anthony Martial ni mmoja wa wachezaji hatari sana aliowahi kukutana nao.

Chelsea wanajianda kutoa ofa ya paundi milioni 88 kumnasa mshambuliaji wa Inter Milan mwenye asili ya Argentina, Mauro Icardi mwezi Januari ili kuongeza nguvu ya kutetea ubingwa wao.

Manuel Lanzini
Mauricio Pochettino anafuatilia mwenendo wa nyota wa klabu ya West Ham, Manuel Lanzini.

Everton watatakiwa kuongeza mshahara wa Sean Dyche mara mbili, walau ufikie paundi milioni 4 au zaidi ili wamshawishi aachane na Burnley.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Real Madrid wako tayari kulipa kiasi cha paundi milioni 71 kumnasa beki wa Paris Saint-Germain, Marquinhos.

Meneja wa West Brom, Tony Pulis yuko katika hali ya presha baada ya mashabiki wa timu hiyo kuomba atimuliwe. (Mirror)

Morata amesema kwamba huwa anajificha katikati ya mashabiki wa Chelsea na kutembea pamoja nao kuelekea nyumbani kwake baada ya mechi.

Kocha wa Ujerumani, Joachim Low anaamini Timu ya Taifa ya Uingereza inaweza kuonyesha ushindani mkubwa kwenye Kombe la Dunia. (Star)

Nyota wa klabu ya Liverpool, Philippe Coutinho atauomba uongozi wa klabu hiyo kukataa ofa yoyote itakayotolewa na Paris Saint-Germain ili afanikiwe kutua Nou Camp. (Daily Mail)

Manchester United wataomba uwezekano wa kuongezwa kwa mikataba ya Juan Mata, Ander Herrera, Ashley Young na Daley Blind hadi itakapofika mwisho wa msimu huu. (Telegraph)

Xherdan Shaqiri
Xherdan Shaqiri amesema wanategemea kufanya sherehe endapo kikosi chao cha Switzerland kitafanikiwa kufuzu kwenda kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2018. (Guardian)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 11 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 11 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/11/2017 10:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.