Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 22 Novemba, 2017

Lionel Messi
Ivan Rakitic amekiri kwamba, uhakika wa Lionel Messi kubaki Barcelona baada ya majira ya joto ni mdogo sana.

Arsene Wenger amemfanya kiungo wa Shalke 04, Leon Goretzka kuwa chaguo lake la kwanza la usajili katika majira ya joto mwakani.

Nacho Monreal ana imani Alexis Sanchez na Mesut Ozil watasalia na klabu yao ya Arsenal angalau hadi mwisho wa msimu.

Thibaut Courtois ameendelea kuipagawisha klabu ya Real Madrid baada ya kugoma kufanya mazungumzo juu ya mkataba mpya hadi mwisho wa msimu huu, ambapo itakuwa imebakia mwaka mmoja kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa.

Gary Megson amewaambia wachezaji wa West Brom kwamba wanatakiwa kubadilika ili klabu yao iepukane na kushuka daraja. (Mirror)

Alan Pardew
West Brom wamekutana na Alan Pardew na kufanya mazungumzo ya awali juu ya uwezekano wa kuchukua nafasi ya meneja wao Tony Pulis aliyefukuzwa kazi.

Jose Mourinho amekanusha taarifa zinazodai kwamba ametofautiana na mchezaji wake, Henrikh Mkhitaryan. (Sun)

Meneja wa Aston Villa, Steve Bruce amesema kuwa Jonathan Kodjia anatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kifundo cha mguu.

Kocha mkuu wa klabu ya Leeds, Thomas Christiansen ameitaja Wolves kuwa klabu bora kwenye Championship. (Express)

Leon Goretzka
Arsenal wataanzisha mazungumzo na klabu ya Schalke 04 juu ya uhamisho wa kiungo Leon Goretzka msimu ujao.

Louis van Gaal hajawasiliana na klabu ya Everton kuhusiana na kuchukua nafasi ya umeneja wa klabu hiyo.

Javairo Dilrosun
Klabu ya Manchester City inapigana kwa hali na mali kubakisha mchezaji wao, Javairo Dilrosun. (Daily Mail)

Kiwango cha Ashley Young msimu huu kimeifanya klabu ya Manchester United impe ofa ya nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 22 Novemba, 2017  Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 22 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/22/2017 01:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.