Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 13 Novemba, 2017

Cristiano Ronaldo na Karim Benzema
Nyota wa klabu ya Real Madrid, Karim Benzema anasema Cristiano Ronaldo ni mbinafsi zaidi yake.

Manchester City na Juventus wanatamka mchezaji wa kati wa Liverpool Emre Can, 23, ambaye mkataba wake utakwisha msimu huu.

Klabu ya Arsenal inakaribia kukamilisha usajili wa nyota wa Lyon, Nabil Fekir kwa   karibu paundi milioni 60 au zaidi. (Star)

Ray Wilkins

Ray Wilkins amesema kuwa Mesut Ozil hastahili kuitwa mchezaji bora wala kuvaa jezi namba 10 ya Arsenal.

Wolves wamemuahidi meneja Nuno Espirito Santo pesa zaidi kumuwezesha kubadili klabu na kuwa mshiriko wa Champions League.

Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Fernando Torres, 33, ana nia ya kurejea Premier League huku Southampton na Newcastle wakitaka kumsaini.

Kiungo wa Liverpool, Emre Can 
Borussia Dortmund wanamvizia kiungo wa Liverpool, Emre Can lakini wana kumbana na ushindani kutoka Juventus. (Mirror)

Manchester United wanataka kumuuza mchezaji wa England Luke Shaw ,22, kwa karibu pauni milioni 20 mwezi Januari. (Times)

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi anatakana klabu hiyo kumtafuta mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham Dele Alli, 21, kabla ya Real Madrid hawajafanya hivyo.

Manchester United wako tayari kulipa pauni milioni 177 kumsaini mchezaji wa kati wa Real Madrid Marco Asensio, 21.(Don Balon)

Patrice Evra amezungumza na vilabu kadha vinavyotaka kumsaini licha ya kumvamia shabiki wa Marseille kwa mujibu wa mwakilishi wake. (Gazzetta dello Sport)
Mshambuliaji wa West Ham, Marko Arnautovic
Mshambuliaji wa West Ham Marko Arnautovic, 28, anasema hatauzwa mwezi Januari. (Kurier)

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 31, anasisitiza kuwa atakuwepo kwenye klabu hiyo. (Independent)

LiverpooL wanataka kutumia paunia milioni 5 kumsaini mchezaji wa miaka 17 wa Wolves Morgan Gibbs-White mwezi Januari. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 13 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 13 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/13/2017 03:54:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.