Loading...

Chelsea kumtumia Batshuayi kama chambo kumnasa nyota huyu


klabu ya Chelsea inaripotiwa kuwa na mpango wa kumtumia Michy Batshuayi kama sehemu ya ofa yao kumnasa nyota wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar.

Kwa mujibu wa ripoti ya Telegraph, Chelsea wako tayari kutoa mchezaji kwenye ofa ya Lemar, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Ligi Kuu ya Uingereza kwa muda mrefu.

Thomas Lemar
Mfaransa huyo alikaribia kusaini mkataba na klabu ya Arsenal kwa paundi milioni 89 siku ya kufungwa kwa dirisha dogo lililopita, lakini dili hilo halikuzaa matunda baada ya Manchester City kushindwa kukamilisha usajili wa Alexis Sanchez.

Licha ya kukosekana kwa Alvaro Morata kwenye mechi ya Huddersfield Town, Batshuayi alikaa benchi, huku Antonio Conte akitoa nafasi kwa Hazard, Willian na Pedro.

Katika msimu huu, Batshuayi amecheza mechi nane pekee, pamoja na kwamba Conte amekuwa akiitafuta mbadala wa kumsaidia Morata. Nyota huyo anaweza kutumiwa kama chambo kufanikisha usajili wa Thomas Lemar kutoka klabu ya Monaco, dili linaloweza kufanikiwa kwa urahisi ikiwa ni pamoja na mapenzi ya mkurugenzi wa michezo wa AS Monaco, Michael Emenalo kwa Mbelgiji huyo.
Chelsea kumtumia Batshuayi kama chambo kumnasa nyota huyu Chelsea kumtumia Batshuayi kama chambo kumnasa nyota huyu Reviewed by Zero Degree on 12/15/2017 11:33:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.