Loading...

Idadi ya waliokufa maji Ziwa Tanganyika yaongezeka

Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) mkoani Kigoma, Amaniel Sekulu amesema miili sita ya watu waliozama katika ajali ya boti kugonga mtumbwi katika Ziwa Tanganyika imeokolewa.

Amesema uokoaji wa miili hiyo ilikumbwa na changamoto kadhaa, ikiwemo wazamiaji kukumbana na hali mbaya ya hewa, mvua za mara kwa mara, mawimbi makubwa na kina kirefu cha maji.

Bw. Sekulu amesema kwamba mpaka sasa idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea Ijumaa iliyopita imefikia 19 kutokana na awali kuopolewa miili 13 na kuongeza kwamba miili hiyo sita imeharibika kutokana na kukaa majini zaidi ya saa 50.

Amesema Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na wananchi wenye ujuzi wa kuogelea ndio waliofanikisha kupatikana kwa miili hiyo.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia Ijumaa ikihusisha boti lililokuwa linatoka Kigoma mjini kwenda Kalya na mtumbwi wa MV Pasaka uliookuwa ukitoka kijiji cha Kalilani kwenda Sunuka.
Idadi ya waliokufa maji Ziwa Tanganyika yaongezeka Idadi ya waliokufa maji Ziwa Tanganyika yaongezeka Reviewed by Zero Degree on 12/25/2017 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.