Loading...

Jose Mourinho hatarini Manchester United


Manchester City iko kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, mbele ya vilabu vingine katika Ligi hiyo ikiwemo na Manchester United, ambayo hadi hivi sasa inaonekana bado haiko tayari kumpatia meneja wake, Jose Mourinho mkataba mpya.
Kwa mujibu wa 'The Mirror', klabu hiyo hadi hivi sasa inashikilia mkataba mpya wa Mreno huyo, habari nyingine zikidai kwamba, vigogo hao hawafurahii namna ambavyo meneja huyo amekuwa akitenda kazi siku za hivi karibuni.

Akiwa ameshika madaraka kama hayo katika klabu za Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid kabla, ambako hakukaa kwa zaidi ya misimu mitatu katika klabu yoyote, Mourinho amekuwa katika mgandamizo mkubwa wakati City ikiwa njiani kubeba taji la msimu huu.

Inasemekana kwamba maauzi ya kitoto ya Jose Mourinho ndio chanzo cha kuwa na migogoro kati yake na wachezaji wakubwa, hapo utakumbuka migogoro yake alipokuwa Chelsea ambako aliwatuhumu wachezaji wake kumsalitki.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 54, alisaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Manchester United mwaka uliopita.
Jose Mourinho hatarini Manchester United Jose Mourinho hatarini Manchester United Reviewed by Zero Degree on 12/29/2017 09:09:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.