Loading...

Kasi ya ubomoaji wa jengo la TANESCO yatakiwa kuongezwa

Waziri wa ujenzi,uchukizi na mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa 
Waziri wa ujenzi,uchukizi na mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameagiza kasi ya ubomoaji wa jengo la TANESCO na ofisi za wizara ya maji iongezwe ili kuharakisha ujenzi wa darara la juu katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

Waziri Mbarawa amefanya ziara katika eneo la Ubungo na maeneo mbalimbali ya barabara ya Morogoro amesema agizo lilotolewa na rais la ubomoaji wa majengo hayo lazima litekelezwe ili kuweza kukamilisha ujenzi uliokusudiwa.

Katika ziara hiyo waziri alipatiwa maelezo kutoka kwa watalaamu mbalimbali kuhusu ujenzi wa barabara hiyo sambamba na hatua zilizofikiwa za kuondoa majengo kama yale ya wizara ya maji.

Ujenzi wa daraja hilo la juu ukikamilika utasaidia kupunguza msongamno wa magari katika makutano ya barabara za Morogoro na Sam Nujoma na Mandela makutano ambayo ni lango kuu na kuingia na kutoka katika jiji la Dar es Salaam.
Kasi ya ubomoaji wa jengo la TANESCO yatakiwa kuongezwa Kasi ya ubomoaji wa jengo la TANESCO yatakiwa kuongezwa Reviewed by Zero Degree on 12/06/2017 08:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.