Loading...

Magogo zaidi 900 yaliyokaa miaka 10 yakutwa bandarini


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla, ameagiza Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii atangaze kujitokeza kwa wamiliki wa magogo 938 yaliyokaa bandarini kwa zaidi ya miaka 10.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla akikagua kontena lililokuwa na magogo hayo bandarini
Kama wamiliki wasipojitokeza, magogo hayo yatakuwa mali ya Serikali Kigwangalla ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandari ya Dar es salaam kufuatia uwepo wa taarifa za uvunaji holela wa magogo nchini, ambapo kuna taarifa kuwa kuna wafanyabiashara wa kigeni wanagawa vifaa vya kuvunia bure kwa ahadi ya kuuziwa mzigo na wahusika.

Aidha taarifa zingine zilizosababisha ziara hiyo kufanyika ni kuwepo kwa taarifa kuwa kuna baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanatoa vibali na kugonga nembo magogo hayo kinyume cha taratibu za kisheria.

Mbali na hayo Dkt Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wamiliki wa makontena 55 yanayodaiwa kuingizwa nchini kutoka Zambia kujitokeza na kuwasilisha nyaraka zao zenye kuthibitisha kama kweli yalivunwa nchini Zambia au la.
Magogo zaidi 900 yaliyokaa miaka 10 yakutwa bandarini Magogo zaidi 900 yaliyokaa miaka 10 yakutwa bandarini Reviewed by Zero Degree on 12/03/2017 04:14:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.