Loading...

Ofisi ya Makamu wa Rais yakanusha kushiriki zoezi la kupanda miti UDOM


Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakanusha tangazo linalosambaa katika Mitandao ya Kijamii linalomhusisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa atashiriki zoezi la kupanda miti kwenye Chuo Kikuu Cha Dodoma siku ya tarehe 1-1-2018. Ofisi ya Makamu wa Rais inapenda kuujulisha umma kuwa tangazo hilo si la kweli na Makamu wa Rais hana ratiba ya kupanda miti kwenye chuo hicho kwa tarehe iliyotajwa.

Ofisi ya Makamu wa Rais yakanusha kushiriki zoezi la kupanda miti UDOM Ofisi ya Makamu wa Rais yakanusha kushiriki zoezi la kupanda miti UDOM Reviewed by Zero Degree on 12/31/2017 03:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.