Loading...

Real Madrid wanataka wachezaji watatu kutoka klabu ya Chelsea


Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Real Madrid wanataka wachezaji watatu kutoka klabu ya Chelsea akiwemo Eden Hazard.

Ripoti za nchini Uhispania zinadai kwamba, vigogo hao wa LaLiga wana nia ya kumsajili Thibaut Courtois na Cesar Azpilicueta pia Eden Hazard

Eden Hazard
Zinedine Zidane amekuwa akihusishwa na Hazard katika siku za hivi karibuni, huku ripoti nyingine zikidai kwamba Mbelgiji huyo bado hajakubali kusaini mkataba mpya na Chelsea.

Mtandao wa Don Balon umeeleza kwamba Hazard anaweza kuondoka Stamford Bridge pamoja na Courtois na Azpilicueta.

Courtois
Ripoti yao inasema kuwa golikipa huyo (Courtois) anahitajika kwenye majira ya joto na atapigania nafasi kwenye kikosi cha kwanza na Kepa Arrizabalaga.

Azpilicueta
Azpilicueta atachukuwa nafasi ya Dani Carvajal, ambaye anadaiwa kushindwa kumshawishi Zidane na kiwango chake.

Chelsea inahofia uwezo wa kifedha wa klabu ya Real Madrid na ina wasiwasi wa kupoteza wachezaji wengi wa muhimu katika kikosi chao, ambao wanaweza kujiunga na vigogo hao wa La Liga.

Akizungumza na waandishi wa habari 
siku ya Ijumaa, meneja wa Chelsea, Antonio Conte alikataa kuzungumzia kuhusu future ya Eden Hazard.

“Jibu langu halitabadilika: Haya ni mazungumzo binafsi kati ya klabu, mchezaji na wakala wake,” alisema.

“Najivunia kuwa naye katika timu yangu, kikosi changu na ninafurahia kufanya naye kazi.

“Ni mtu mzuri sana, mwenye nafasi kubwa ya kufanya mabadiliko.”
Real Madrid wanataka wachezaji watatu kutoka klabu ya Chelsea Real Madrid wanataka wachezaji watatu kutoka klabu ya Chelsea Reviewed by Zero Degree on 12/31/2017 04:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.