Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 21 Decemba, 2017

Gabriel Jesus
Gabriel Jesus anategemewa kukubali kusaini mkataba wa miaka mitano Manchester City ambao utamwingizi paundi 100,000 kila wiki.

Everton wako tayari kutoa ofa kwa ajili ya kumnasa Theo Walcott kufuatia madai ya kwamba anataka kuondoka Arsenal ili kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza kombe la dunia mwakani.

West Ham wameiuliza klabu ya Sevilla kama kiungo wao, Steven Nzonzi atakuwa huru kuondoka kwa mkopo mwezi Januari. (Daily Mail)

Klabu ya Chelsea ina matumaini ya kuvunja rekodi kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari kwa kuwasajili Thomas Lemar na Ross Barkley.

Arsenal wako kwenye mchakato wa kumsajili kiungo wa Lyon, Houssem Aouar.

Nyota wa Inter Milan, Joao Mario anakiri kwamba hafurahii kitendo cha kukosa muda wa kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Meneja wa klabu ya Everton, Sam Allardyce ana mpango wa kumsajili beki wa Crystal Palace, James Tomkins.

Solomon Kvirkvelia
West Brom na Leicester City zitachuana kuwania saini ya nyota wa Lokomotiv Moscow, Solomon Kvirkvelia.

Connor Goldson anatarajiwa kurejea kwenye Ligi Kuu ya Uingereza katika mechi dhidi ya Watford siku ya Jumamosi, mwezi 10 baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo. (Sun)

Manchester City wamefikia makubaliano na klabu ya Libertad ya Paraguay kuhusiana na uhamisho wa kiungo wao, Jesus Medina kwa ada ya paundi milioni 3.

Mark Hughes yuko kwenye hatari ya kuwa meneja wa saba kufukuzwa kazi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kama atapoteza mechi dhidi ya West Brom siku ya Jumamosi. (Guardian)

Paris Saint-Germain wako tayari kutoa ofa ya paundi milioni 25 mwezi Januari kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez kujaribu kutibua mikakati ya Manchester City. (Express)


Kenedy
Newcastle wamefanikiwa kumnasa kiungo wa klabu ya Chelsea, Kenedy kwa mkopo.

Klabu ya Swansea inajaribu kumshawishi Louis van Gaal awe meneja wao mpya.

Alexis Sanchez atapewa ofa ya kulipwa msahahara wa paundi 400,000 kwa wiki ili aachane na klabu ya Arsenal na kujiunga na Manchester City.

David Luiz amejitoa kujiunga na klabu ya Barcelona, klabu hiyo ikiwa kwenye mchakato wa kumtafuta mbadala wa Javier Mascherano.

Ndoto za Daniel Sturridge kupigania nafasi kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza zinaweza kufifia baada ya Jurgen Klopp kuwa kwenye maandaliza ya kumbakisha nyota huyo Anfield kwa kipibdi chote cha kilichobaki katika msimu huu.

Klabu za West Brom, West Ham na Crystal Palace ziko kwenye ushindani wa kuwania saini ya golikipa wa Manchester United, Sam Johnstone.

Klabu ya Everton ina nia ya kumsajili golikipa wa Espanyol, Roberto, anayedaiwa kuwa na thamani ya paundi milioni 1 na kwa sa sa anaichezea klabu ya Malaga kwa mkopo.

Napoli wana matumaini makubwa ya kumsajili beki wa Manchester United, Matteo Darmian.

Tottenham ina tazamia kumsajili nyota wa klabu ya Lyon, Maxwel Cornet, ambaye anadaiwa kuwa na thamani ya paundi milioni 7. (Mirror)

Swansea wanamfuatilia aliyekuwa kocha wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal ili awe meneja wao mpya.

Beki wa klabu ya Watford, Brice Dja Djedje, amabye hajafanikiwa kuichezea klabu hiyo kwa takribani miezi 17, anatarajiwa kuondoka na kujiunga na kalbu ya Lens ya Ufaransa.

Brentford wamehakikishiwa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Timua y Taifa ya Denmark, Emiliano Marcondes kama mchezaji huru kutoka Nordsjaelland mwezi ujao.

QPR imemruhusu mshambuliaji mwenye asili ya Kifaransa, Yeni Ngbaokoto kuondoka mwezi Januari. (Star)

Klabu ya Barcelona iko tayari kulipa kiasi cha paundi milioni 132 kumnasa kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho katika dirisha dogo la uhamisho mwezi Januari. (Sport)

Thomas Lemar
Lemar anadaiwa kutaka kuhamia katika klabu ya Liverpool badala ya kwenda Stamford Bridge ama Arsenal.

Tony Pulis na Leon Britton ni miongoni mwa makocha walioko mstari wa mbele kuchukua nafasi ya Paul Clement katika klabu ya Swansea. (Independent)

Klabu ya Estoril inafanya mahesabu ya kujaribu kumsajili beki wa klabu ya Rangers, Fabio Cardoso. 
(Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 21 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 21 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/21/2017 06:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.