Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 28 Decemba, 2017

Paulo Dybala
Klabu ya Juventus imeitaka Manchester United kulipa kiasi cha paundi milioni 133 ili kumpata Paulo Dybala. (Express)


Tottenham watafanya mabadiliko kwenye mfumo wao wa ulipaji mishahara ili  kumfanya Harry Kane asiondoke.

Manchester City inategemewa kufanya maboresho kwenye safu yao ya ulinzi wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari, Jonny Evans na Ryan Bertrand wakiwa vinara kwenye orodha ya wachezaji wanaowahitaji.

West Ham wanatarajiwa kutoa ofa ya paundi milioni 25 kwa ajili ya uhamisho wa beki wa klabu ya Swansea, Alfie Mawson. (Daily Mail)

Jack Wilshere anatambua kwamba yuko kwenye hatua nzuri kurejesha kiwango chake akipigania kupata mkataba mpya Arsenal.

Abdoulaye Doucoure
Watford wako tayari kumfanya kiungo wao, Abdoulaye Doucoure kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi ndani ya klabu hiyo kwa kumpa mkataba mpya wa miaka mitano.

Craig Dawson anasistiza kwamba West Brom inaweza kuitikisa Arsenal kwa mara nyingine tena, licha ya kwamba kikosi chao kina hali mbaya. (Mirror)

Vigogo wa Shirikisho la Soka la Uingeleza (FA), wana amini kwamba taifa hilo liko kwenye nafasi nzuri kushinda nafasi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2030.

Atletico Madrid wako tayari kumwachia nyota anayewindwa na klabu ya Chelsea, Yannick Carrasco aondoke mwezi ujao.

Gabriel Pires
West Ham wanafanya mpango wa kumnasa nyota wa klabu ya Leganes, Gabriel Pires mwezi Januari.

Klabu ya Everton inatarajiwa kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Besiktas, Cenk Tosun kwa paundi milioni 25. (Sun)

Sandro Ramirez anaweza kuondoka Everton baada ya klabu ya Valencia kuonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo.


Jack Wilshere anaweza kuhitajika kushusha kiwango cha mshahara anachohitaji ili aweze kupata mkataba mpya Arsenal.

Mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata amemshukuru Marcos Alonso kwa kumsaidia kuizoea klabu yake mpya ndani ya muda mfupi. (Star)

Harry Kane amaezungumzia shauku yake ya kutaka kushinda mataji akiwa na klabu ya Tottenham kufuatia kuvunja rekodi ya magoli mwaka 2017.

Yannick Bolasie
Yannick Bolasie anakiri kwamba, safu ya ushambuliaji katika klabu ya Everton imekuwa butu chini ya uongozi wa Sam Allardyce, lakini ana uhakika kwamba timu hiyo itafanya maboresha katika safu hiyo. (Guardian)


Aliyekuwa nyota wa klabu ya Real Madrid, Angel Di Maria anakaribia kujiunga na Barcelona. 

Beki wa Southampton, Virgil van Dijk anakaribia kuvunja rekodi na kuwa beki ghali zaidi katika historia ya soka kwa kujiunga na Liverpool kwa dau la paundi milioni 75. (ESPN)

Kwa mujibu wa mtazamo wa Hugo Lloris, Harry Kane anaweza kushindanishwa na Lionel Messi pamoja na Cristiano Ronaldo. (Telegraph)

Klabu ya Celtic itaingiza zaidi ya paundi milioni 6 baada Southampton kukubali ofa ya Liverpool kwa ajili ya uhamisho wa Virgil van Dijk.
 (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 28 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 28 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/28/2017 12:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.