Loading...

Dau la pauni milioni 75 kumpeleka Virgil van Dijk Anfield


Beki wa kati wa klabu ya Southampton, Virgil van Dijk atajiunga na Liverpool kwenye dirisha dogo la usajili tarehe mosi mwezi Januari kwa dau litakalovunja  rekodi ya kimataifa ya pauni milioni 75.

Virgil van Dijk
Muholanzi huyo alitarajiwa kujiunga na Liverpool msimu uliopita baada ya kuomba uhamisho kutoka kwa klabu yake, lakini uhamisho huo haukufaulu baada ya Southampton kuishutumu Liverpool kufanya mawasiliano na mchezaji huyo kinyume na sheria.

Ada hiyo ni kubwa, ambayo itakuwa ya kwanza kulipwa kwa ajili ya usajili wa beki katika historia ya soka - mwezi Julai, Manchester City iliilipa Monaco kiasi cha paundi milioni 52 kwa ajili kumnasa Mbeligiji Benjamin Mendy.

Katika taarifa yake, Van Dijk amesema, ''amefurahia'' kusaini mkataba na klabu hiyo na kukiri kwamba amekuwa na wakati mgumu '' kwa miezi michache iliyopita'' akiwa Southapton.

Beki huyo aliachwa nje ya kikosi cha timu yake kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza, Southampton iliposhindwa kwa goli 5-2 dhidi ya Tottenham Jumanne iliyopita.
Dau la pauni milioni 75 kumpeleka Virgil van Dijk Anfield Dau la pauni milioni 75 kumpeleka Virgil van Dijk Anfield Reviewed by Zero Degree on 12/28/2017 12:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.