Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 29 Decemba, 2017


Florentino Perez anataka kuhakikisha Real Madrid inafanikiwa kumnasa Neymar kutoka PSG kwenye majira ya joto ili kuiumiza klabu ya Barcelona.

Lionel Messi hataki Barcelona imsajili kiungo wa Gremio, Arthur na badala yake imkazanie Philipe Coutinho.

Ozil ana masharti mawili kwa uongozi wa klabu ya Barcelona ili akubali kusaini mkataba na klabu hiyo. (Don Balon)

Klabu ya Juventus imekataa ofa ya pauni milioni 70 iliyoambatana Henrikh Mkhitaryan kutoka Manchester United kwa ajili ya Paulo Dybala.

Arsenal itashindana na Manchester City kuwania saini ya nahodha wa West Brom, Jonny Evans kwenye dirisha la usajili mwezi Januari.

Jack Wilshere amesema kwamba ana shauku kubwa ya kuanza mazunguzo na klabu ya Arsenal juu ya mkataba mpya.


Jose Mourinho anahofu kwamba kasi ya Romelu Lukaku imepungua kufuatia ongezeko kubwa la misuli yake tangu ajiunge na Manchester United.

Meneja wa Stoke City, Mark Hughes anasistizi kwamba mshambuliaji wa PSG,  Jese anataka mafanikio kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. (Sun)

Southampton wana nia ya kuwasajili Daniel Sturridge, Alfie Mawson na Ryan Sessegnon kwa kutumia fedha waliyoipata baada ya kumuuza Virgil van Dijk.

Manchester City watarejea tena sokoni kujaribu kutafuta saini ya beki wa klabu ya Real Sociedad, Inigo Martinez au Jonny Evans. (Telegraph)

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Atletico Madrid, Miguel Angel Gil Marin, klabu hiyo itajaribu kumbakisha Antoine Griezmann kwenye majira ya joto.

Klabu ya Juventus imegoma kupokea ofa kutoka Manchester United ya pauni milioni 70 na nyongeza ya Henrikh Mkhitaryan kama sehemu ya ofa hiyo kwa ajili ya Paulo Dybala. (ESPN)

Arsene Wenger hana hofu ya kumpoteza Alexis Sanchez kwenye disha dogo la usajili mwezi Januari. (Sky Sports)

Theo Walcott
Southampton wanataka kumrejesha Theo Walcott kutoka Arsenal wakati fedha kutoka Liverpool kwa ajili ya Virgil van Dijk zitakapowasili.

Chelsea wana uhakika wa kumshawishi Thibaut Courtois asaini mkataba mpya wa miaka mitano kumaliza mipango ya Real Madrid kutaka kumsajili.

Klabu ya West Ham inataka kumsajli Joe Allen na Lamine Kone kwenye dirisha dogo la mwezi Januari. (Mirror)

Barcelona wanaamini klabu za Manchester zitaweza kulipia fedha kwa ajili ya kuvunja mkataba wa Samuel Umtiti.

Everton watatafuta mwanya wa kumnasa kiungo wa Sevilla, Steven N'Zonzi ndani ya masaa 48 yajayo.

Leicester City wamefanya mazungumzo na klabu ya Benfica kuhusu uhamisho wa Andre Almeida.

Huddersfield Town wamezungumza na Monaco kuhusu Almamy Toure.

Brighton wanahofia West Ham kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya mshambuliaji wa Celtic, Moussa Dembele.

Real Madrid wamemchunguza Ryan Sessegnon katika klabu ya Fulham msimu huu lakini bado anategemewa kujiunga na Tottenham.

Yannick Carrasco
Yannick Carrasco ana mpango wa kuondoka katika klabu ya Atletico Madrid mwezi ujao. (Daily Mail)

Ripoti zinadai kwamba, klabu ya Real Madrid inajianda kumnasa beki wa Manchester United, Daley Blind. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 29 Decemba, 2017  Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 29 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/29/2017 02:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.