Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 8 Decemba, 2017

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi
Lionel Messi amesema kwamba atastaafu kucheza soka la kimataifa endapo Argentina itafanya vibaya kwenye kombe la Dunia mwaka 2018.

Chelsea wanamtaka Leon Bailey wa Bayer Leverkusen kwa paundi milioni 20 mwezi Januari, lakini inakumbana na ushindani kutoka klabu ya Barcelona.

Philippe Coutinho amekiri kwamba hana uhakika wa kusalia katika klabu ya Liverpool, Barcelona ikijiandaa kutoa ofa ya paundi milioni 127 mwezi januari. (Sun)

Mechi ya wapinzani wa jadi wa mji wa Manchester siku ya Jumapili, inatarajiwa kuwa ya gharama zaidi na itakayotazamwa na watu wengi zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Klabu ya Swansea City itaendeleza imani yake kwa meneja Paul Clement na kumpa muda wa kuijenga Timu kwenye dirisha dogo la usajili.

Pep Guardiola na Sergio Aguero
Pep Guardiola ana matumaini kwamba Sergio Aguero anaweza kuitumia mechi yao dhidi ya Manchester United kurejea katika kiwango chake. (Telegraph)

Sam Allardyce anataka kutoa ofa ya paundi milioni 60 kumnasa nyota wa klabu ya Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang.

Zlatan Ibrahimovic, Marouane Fellaini na Phil Jones wote wanatarajiwa kuwa 'fit' kwa ajili ya mechi ya Manchester United dhidi ya Manchester City Jumapili.

Klabu ya Swansea iko inafanya mpango wa kumnasa Tony Pulis.

Chelsea wako katika ushindani mkubwa na klabu ya Barcelona kuwania saini ya kiungo wa Gremio, Arthur.

Mike Ashley na Amanda Staveley walikutana mjini London kuzungumzia suala la kuuziana klabu ya Newcastle. (Mirror)

Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United, Andrei Kanchelskis amesema kwamba Pep Guardiola ni zaidi ya Jose Mourinho.

Meneja wa West Ham, David Moyes ameamua kumuacha Joe Hart nje na kumchagua Adrian akae golini kwenye mechi yao dhidi ya Chelsea wikendi.

Dani Carvajal
Dani Carvajal ataikosa mechi ya kwanza ya Real Madrid kwenye hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa baada ya kufungiwa na UEFA kujitafutia kadi ya njano makusudi. (Daily Mail)

Theo Walcott ana matumaini kwamba amefanya kila liwezekanalo kumshawishi  Arsene Wenger amrejeshe katika mipango yake kwenye mechi ya Ligi ya Europa dhidi ya Bate Borisov, Arsenal ilipoibuka na ushindi wa bao 6-0. (Express)

FIFA wamemwondoa mchunguzi aliyekuwa amewekwa kwa ajili ya kumfanyia uchunguzi kiongozi wa Kombe la Dunia Urusi, Vitaly Mutko.

Manchester City, Manchester United zinaweza kupanga ratiba ya kukutana tena dimbani nje ya Uingereza kwenye majira ya joto, kama ilivyofanyika mwezi Julai nchini Marekani. (Guardian)

Meneja wa klabu ya West Brom, Alan Pardew amesema atafanya mpango wa kumtafuta mbadala wa nahodha wake, Jonny Evans mwezi January. 
(Star)

Yaya Toure
Yaya Toure anadai kwamba Manchester United watakuwa na hofu ya kuikabili Manchester City siku ya Jumapili. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 8 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 8 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/08/2017 01:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.