Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 16 Decemba, 2017

Mohamed Salah
Zinedine Zidane amezungumzia mpango wa klabu ya Real Madrid kujaribu kumnasa Mohamed Salah baada ya kukiri kwamba nyota huyo wa Liverpool ni miongoni mwa wachezaji anaowakubali sana.

Diego Maradona amemuonya Cristiano Ronaldo kuhusiana na kile anachodai kwamba yeye ni bora zaidi kuliko katika historia ya soka na kumwambia nyota huyo wa klabu ya Real Madrid bado anatakiwa kukaza buti.

Henrikh Mkhitaryan anakaribia kuondoka Manchester United baada ya kutofautiana na meneja wa klabu hiyo, Jose Mourinho. (Sun)

Batshuayi, 24, anatarajia kuondoka Chelsea mwezi ujao kwa mkopo kupunguza hofu ya kupoteza nafasi yake katika kikosi cha Ubelgiji kitakachocheza katika kombe la dunia.

Mousa Dembele
Kiungo wa klabu ya Tottenham, Mousa Dembele amegundua mali iliyopotea yenye thamani ya £1m katika dari la nyumba yenye miaka 700 huko Antwerp.

Arsenal itafanya mazungumzo ya kandarasi mpya na mchezaji wa kiungo cha kati, Jack Wilshere kabla ya mwisho wa mwezi. (London Evening Standard)

Chelsea wana jiandaa kuoa ofa inayoambatana na mchezaji kumnasa nyota wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar ambaye anakisiwa kuwa na thamani ya paundi milioni 80 na wako tayari kumjumuisha straika wa Ubeligji, Michy Batshuayi ndani ya ofa hiyo.

Arsenal wanaweza kupoteza wachezaji nane kwenye majira ya joto, Arsene Wenger akijiandaa kushuhudia mtikisiko ndani ya kikosi chake kwa mara ya kwanza. (Mirror)

Ripoti zinadai kwamba Barcelona imeambia ilipie kiasi cha paundi milioni 127 kwa ajili ya kumnasa nyota wa Liverpool, Philippe Coutinho - lakini mazungumzo bado yanaendelea. (Express)

Kiungo wa Timu ya Taifa ya Armenia, Henrikh Mkhitaryan ameachwa nje ya kikosi cha na Jose Mourinho baada ya kuzuka mzozo kati yao wakati wa tathmini ya mechi katika uwanja wao wa mazoezi mwezi uliopita. (ESPN)

Domingos Quina
West Ham imejiandaa kumbakisha Domingos Quina, huku Liverpool ikiwa mstari wa mbele kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya nyota huyo. (Daily Mail)

Arsene Wenger anakiri kwamba Ligi Kuu ya Uingereza imekuwa ngumu sana kwake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita - ikiwa timu nyingi zaidi zinatumia mfumo wa kupaki basi. (Star)

Jose Mourinho anasema kuwa atamruhusu mchezaji yeyote atakaye taka kuondoka Manchester United kwa bei inayokubalika mwezi Januari, taarifa ambayo inatoa majibu juu ya uvumi wa msatakabali wa maisha ya soka ya Henrikh Mkhitaryan na Luke Shaw.

Meneja wa klabu ya Everton, Sam Allardyce anasema uhusiano wake na mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Steve Walsh, unaweza kuhakikisha mfumo wa usajili wa wachezaji unazaa matunda Goodison Park. (Telegraph)

Carlo Ancelotti
Carlo Ancelotti atarudi Stamford Bridge na kuwa meneja wa Chelsea kabla ya kuanza kwa msimu mpya. (Record)

Gareth Bale na Aaron Ramsey wanataka Carl Robinson, ambaye ni meneja wa Whitecaps, kuchukua nafasi iliyoachwa na Chris Coleman kama meneja wa Timu ya Taifa ya Wales. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 16 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 16 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/16/2017 06:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.