Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 23 Decemba, 2017
Gareth Bale |
Gareth Bale ameiambia Real Madrid kuwa anataka kuondoka Bernabeu na kurejea kwenye Ligi Kuu ya Uingereza katika klabu ya Manchester United.
Jose Mourinho anatazamia kumsajili winga wa klabu ya Monaco, Thomas Lemar, na ameorodhesha wachezaji wengine kadhaa inayowajumuisha Justin Kluivert, Christian Pulisic na Malcom.
Chelsea wanafanya mpango wa kubadilisha wachezaji utakaomfanya David Luiz ahamie AC Milan na Leonardo Bonucci atue Stamford Bridge.
Sam Allardyce anasema kwamba anataka kusajili mshambuliaji mpya na beki wa pembeni mwezi Januari, lakini anadai hatamsajili Steven N'Zonzi kwani klabu ya Everton tayari ina viungo wa kutoshaa.
Ivan Rakitic anasema kuwa Barcelona itamkaribisha kwa mikono miwili nyota wa klabu ya Liverpool, Philippe Coutinho.
Manchester United na Liverpool zote kwa pamoja zina nia ya kumsajili nyota wa klabu ya Barcelona, Sergi Roberto. (Star)
Sergio Aguero |
Mstakabali wa maisha ya soka ya Sergio Aguero katika klabu ya Manchester City uko shakani baada ya nyota huyo kuonyesha kukasirishwa na kitendo cha Pep Guardiola kushindwa kumchezesha kwenye mechi kubwa. (Times)
Antonio Conte ana sahuku kubwa ya kutua Real Madrid kama meneja mpya.
Wachezaji wa klabu ya Manchester United wanategemea kuona kati ya Antoine Griezmann au Gareth Bale anasaini mkataba wa kujiunga klabu hiyo mwishoni mwa msimu.
Bournemouth wameikataa ofa ya West Ham ya paundi milioni 8 kwa ajili ya kiungo wao, Harry Arter, lakini klabu hiyo ina mapango wa kurejea upya na ofa iliyoboreshwa dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi Januari.
Rais wa klabu ya Lazio, Claudio Lotito anasema kwamba hatamzuia Stefan de Vrij kujiunga na Liverpool kama yeye binafsi ataamua kufanya hivyo wakati mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu.
Moussa Dembele |
klabu ya Celtic iko tayari kumuuza Moussa Dembele kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari, huku Everton na West Ham zikiwa mstari wa mbele kuwania saini yake. (Express)
David Moyes hataki kuzungumzia suala la kuongeza mkataba katika klabu ya West Ham hadi msimu utakapomalizika, licha ya kwamba mkataba wake wa sasa unamalizika kwenye majira ya joto.
Crystal Palace wanawinda saini ya mshambuliaji wa FC Basel, Mohamed Elyounoussi na golikipa wa Gillingham, Tomas Holy kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari.
Kwa mujibu wa Antonio Conte, Wayne Rooney atakuwa alivunjika moyo hadi kufikia hatua ya kuamua kustaafu kucheza soka la kimataifa. (Daily Mail)
Manchester United wanajiandaa kutoa ofa ya paundi milioni 25 kwa ajili ya kumnasa chipukizi wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon, na wako tayari kumruhusu Luke Shaw aondoke zake.
Manchester United wanajiandaa kutoa ofa ya paundi milioni 25 kwa ajili ya kumnasa chipukizi wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon, na wako tayari kumruhusu Luke Shaw aondoke zake.
Tottenham wanaweza kumwachia Georges-Kevin Nkoudou aondoke kwa mkopo ili nafasi yake kwenye Ligi ya Mabingwa ichukuliwe na Erik Lamela aliyerejea kwenye kiwango chake.
Rafael BenÃtez ametoa tarehe ya ukomo kwa mmiliki wa klabu ya Newcastle, Mike Ashley kuongeza nguvu kikosini mwezi Januari. (Guardian)
Arsenal wako mbele ya Manchester United kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya beki wa klabu ya Juventus, Daniele Rugani na watatoa ofa ya paundi milioni 34.5 mwezi Januari.
West Ham inatarajiwa kutoa ofa ya paundi milioni 20 kwa ajili ya beki wa klabu ya Swansea, Alfie Mawson wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa.
Manuel Akanji |
Jurgen Klopp atashindana na klabu yake ya zamani, Borussia Dortmund kuwania saini ya beki wa FC Basel, Manuel Akanji. (Sun)
Romelu Lukaku ameacha kushangilia magoli kwa sababu hafurahii kitendo cha Zlatan Ibrahimovic kumlazimisha kucheza pembeni, na pia ana hasira kwanini Jose Mourinho haingilii kati suala hilo.
Mauricio Pellegrino amemwambia Virgil van Dijk kwamba hana nafasi tena Southampton.
Mauricio Pellegrino anasistiza kwamba Dele Alli bado "ni wa muhimu sana" kwa Tottenham, licha ya kwamba kiwango chake kimeshuka.
Manchester United inashindana Liverpool pamoja Arsenal kuwania saini ya winga wa Monaco, Thomas Lemar.
Arsenal wanafanya mpango wa kumnasa nyota wa klabu ya Barcelona, Jose Arnaiz kwa paundi milioni 17.7. (Mirror)
Meneja wa Everton, Sam Allardyce amesema kwamba atajaribu kufanya usajili wa wachezaji wawili kwenye dirisha dogo la usajili baada ya kupewa fedha za kutumia na mmiliki wa klabu hiyo Farhad Moshiri. (Independent)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 23 Decemba, 2017
Reviewed by Zero Degree
on
12/23/2017 07:54:00 PM
Rating: