Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 19 Decemba, 2017

Wilfried Zaha
Manchester City wako tayari kushindana na klabu za Arsenal na Chelsea katika kuwania saini ya Wilfried Zaha.

Klabu ya Inter Milan ina matamanio ya kumnasa kiungo wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan kwa mkopo mwezi Januari.

Swansea City wamekubali kulipa kiasi cha paundi milioni 2 kwa ajili ya kumnasa beki wa klabu ya Barnsley, Andy Yiadom.

Southend United wanatarajia kupokea ofa ya tano kutoka klabu ya Sheffield United kwa ajili ya kiungo wao, Ryan Leonard. (Mirror)

Mikel Arteta
Mikel Arteta anatarajiwa kuchukua nafasi ya Arsene Wenger kama meneja wa klabu ya Arsenal.

David Luiz ana matumaini ya kuboresha kiwango chake kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo mwezi Januari. (Telegraph)

Tony Pulis yuko tayari kurejea Stoke City ili kuipesha klabu hiyo na kushuka daraja.

Arsenal wako tayari kuboresha safu yao ya ulinzi kwa kumnasa beki wa klabu ya Chelsea, David Luiz anayekadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 25.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anatazamia kumsajili nyota wa klabu ya Mainz, Abdou Diallo. (Sun)

Meneja wa klabu ya West Ham, David Moyes amechukizwa na uamuzi wa Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) kumwadhibu Manuel Lanzini kwa kosa la kujiungasha kwenye mechi ya klabu hiyo dhidi ya Stoke City.

Henrikh Mkhitaryan
Manchester United inahitaji zaidi ya paundi milioni 35 ili kumwachia Henrikh Mkhitaryan.

Klabu za Aston Villa na Sheffield United zimeulizia kuhusiana na mstakabali wa mshambuliaji wa Leicester, Leonardo Ulloa, lakini inaonekana meneja wa klabu hiyo, Claude Puel ana matamanio makubwa ya kumbakisha kikosini raia huyo wa Argentina. (Daily Mail)

Scott Brown amesistiza kwamba, wachezaji wa Celtic watajifunza kutoka kipigo cha kushitukiza dhidi ya Hearts.

Manchester City wako tayari kuingia kwenye ushindani na Arsenal kuwania saini ya beki wa klabu ya Chelsea, David Luiz. (Express)

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amesema kuwa hayuko tayari kuishuhudia Manchester City ikimsajili beki wa klabu ya Southmpton, Virgil van kiurahisi. (Goal)

Arsene Wenger anafikiria kumpa ofa nahodha wa klabu ya Manchester City, Vincent Kompany ikiwa vinara hao wa Ligi Kuu ya Uingereza watajaribu kwa mara nyingine tena kumsajili Alexis Sanchez mwezi Januari.

Sol Campbell 
Sol Campbell ana tamani kurejea Portsmouth kama sehemu ya benchi la ufundi la klabu hiyo.

Brighton watakataa ofa yoyote kutoka Rangers wa ajili ya kumnasa winga wao, Jamie Murphy kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Star)

Henrikh Mkhitaryan anaweza kurejea Borussia Dortmund, kurudia uhamisho ambao klabu hiyo ya Bundesliga kumrejesha Shinji Kagawa klabuni baada ya kununuliwa na Manchester United.

Angel Rangel anasema kwamba, klabu ya Swansea City haina njia ya kusonga mbele tena. (Independent)

Mwenyekiti wa klabu ya Aberdeen, Stewart Milne ameahidi kumpa fedha za kutosha meneja wa klabu hiyo, Derek McInnes kwa ajili ya usajili wa wachezaji kwenye dirisha dogo mwezi Januari baada ya kumshawishi asiondoke katika klabu ya Rangers. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 19 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 19 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/19/2017 06:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.