Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 17 Decemba, 2017

Iker Casillas 
Aliyekuwa golikipa wa klabu ya Real Madrid na Timu ya Taifa ya Uhspania, Iker Casillas amemwambia wakala wake amfanyie mpango wa kuhamia Ligi Kuu ya Uingereza mwezi ujao.

Jonny Evans anaweza kurejea Manchester Utd kutoka West Brom kwenye dirisha dogo mwezi Januari kufuatia Eric Bailly kupata majeraha.

Klabu ya Rangers inaweza kuendelea na mchakato wa kusaka meneja mpya hadi mwaka ujao baada ya Tony Pulis kusema anataka kuwa mapumzikoni katika kipindi cha Christmas.

Menea wa Everton, Sam Allardyce ana fanya mpango wa kumnasa straika wa klabu ya Crystal Palace, Christian Benteke mwezi Januari.

Klabu ya Chelsea iko tayari kumuuza David Luiz kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari, baada ya beki huyo kutofautiana na Antonio Conte.

Klabu za Arsenal na Chelsea ziko kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini nyota wa klabu ya Bayer Leverkusen, Leon Bailey.

Ryan Sessegnon
Tottenham wanakumbana na faini ya uhamisho ya paundi milioni 20 wakiwa kwenye mchakato wa kumsajili nyota wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon aje kuwa mbadala wa nyota anayewaniwa na klabu ya Manchester United, Danny Rose.

Fabian Delph anatarajia kusaini mkataba mpya Manchester City endapo atakuwa kwenye kiwango cha juu hadi mwisho wa msimu huu.

Alan Pardew ana fanya mpango wa kuitisha mazungumzo na mmiliki wa klabu ya West Brom, Guochuan Lai kuhusiana na suala zima la uhamisho wa wachezaji. (Mirror)

Raheem Sterling alifanyiwa vitendo vya ubaguzi wakati alipofika kwenye uwanja wa mazoezi wa Manchester City kabla ya mechi yao dhidi ya Tottenham siku ya Jumamosi.

West Brom wanatarajia kumpa ofa ya mkataba mpya wenye thamani kubwa beki wao Jonny Evans kumfanya akatae ofa zitakazotolewa na Manchester City na Arsenal. (Telegraph)

Manchester United wanatazamia kutoa ofa ya kuanzia paundi milioni 30 kwa ajili ya kumnasa nyota wa Bordeaux, Malcolm kwenye dirisha dogo mwezi Januari.

Neymar akiwa na baba yake mzazi
Mategemeo ya Neymar kuhamia Real Madrid yanaweza kuwa makubwa baada ya ripoti za Spain kudai kwamba baba mzazi wa nyota huyo amekutana na Rais wa klabu hiyo. (Times)

Dominic Calvert-Lewin atakuwa na wakati mgumu kupigania nafasi yake katika kikosi cha Everton endapo meneja wa klabu hiyo, Sam Allardyce ataleta straika mpya mwezi ujao.

Meneja wa Everton, Sam Allardyce atahitajika kuachana na kiungo wake mmoja kama atataka kumsajili Steven N'zonzi mwezi Januari.

Klabu ya Swansea inatarajiwa kuanzisha upya mpango wake wa kumsajili nyota wa West Brom, Nacer Chadli mwezi Januari. (Star)

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp anasema kuwa alishinikizwa na mawakala wake kumsajili Mohamed Salah msimu huu baada ya kuhofia umri wa winga huyo wa Misri kuwa mdogo sana kuweza kuhimili mikiki ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Hofu ya kushuka daraja inaongeza ugumu kwa Amanda Staveley kuinunua klabu ya Newcastle United.

Mauricio Pellegrino amekiri kwamba, beki wa Southampton, Virgil van Dijk anaweza kuondoka mwezi Januari.

Philipp Max
Manchester City wamemfanyia uchunguzi beki wa klabu ya Augsburg, Philipp Max, ikiwa ni mikakati ya Pep Guardiola kutafuta beki atakayechukua nafasi ya Benjamin Mendy aliyepata majeraha. (Daily Mail)

Antonio Conte anatarajiwa kujaribu kumsajili beki wa klabu ya Juventus, Alex Sandro mwezi Januari.

Brendan Rodgers anatambua kwamba wachezaji wengi wa Scotland wangeweza kuichezea Celtic kama wangekuwa na mawazo yenye nguvu. (Express)

Jurgen Klopp amwembia Daniel Sturridge kuwa yuko huru kuondoka Liverpool mwezi Januari kama atataka kupigania nafasi kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia.

Swansea wataachana na Paul Clement na kumpa madaraka Leon Britton kama viongozi wa klabu wataamua kufanya mabadiliko.

Bournemouth inamtaka chipukizi wa klabu ya Chelsea, Dujon Sterling mwezi Januari.

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez amekataa mshahara wa paundi 400,000 kwa wiki nchini China kulinda nia yake ya kuhamia Manchester City.

Klabu ya West Ham inamtaka Harry Arter na iko tayari kulipa kiasi cha paundi milioni 15 kwa ajili ya kumnasa nyota huyo wa klabu ya Bournemouth mwezi Januari.

Meneja wa klabu ya Newcastle, Rafa Benitez anatarajiwa kutoa ofa kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa Liverpool, Danny Ings.

Golikipa wa Liverpool, Danny Ward atakataa ofa ya kuhamia Sunderland kwa mkopo. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 17 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 17 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/17/2017 06:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.