Loading...

Waziri Kigwangalla atambulisha Jeshi lake


Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ametumia vyema mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa sheria kwa kuanzisha Jeshi Usu ili kuimarisha utendaji wa shughuli za wizara hiyo.

Kigwangalla amesema kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa kazi za Wizara ya Maliasili na Utalii, sheria namba 5 ya mwaka 2009 inampa mamlaka Waziri mwenye dhamana kuanzisha Jeshi Usu.

Waziri Kigwangalla ameyabainisha hayo kwenye hitimisho la mafunzo ya viongozi mbalimbali wasimamizi wa mapori ya akiba, mapori tengefu, wahifadhi na maofisa Wanyamapori, yaliyofanyika katika kituo cha Mlele, Mkoani Katavi.


“Tumeamua kujibadilisha sasa kwenda kuwa Jeshi Usu ili kuongeza tija na ufanisi katika kazi zetu”, amesema Kigwangalla.

Aidha katika Jeshi hilo Waziri Kigwangalla amemumwagia sifa dada mmoja, ambaye siku ya kwanza ya mafunzo alipewa silaha akaangua kilio kuwa hawezi na anaogopa kuitumia lakini jana kwenye mafunzo ndiye alikuwa wa kwanza kwa shabaha.

Source: eatv
Waziri Kigwangalla atambulisha Jeshi lake Waziri Kigwangalla atambulisha Jeshi lake Reviewed by Zero Degree on 12/17/2017 04:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.