Loading...

Anayetarajiwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Chelsea huyu hapa

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte
Kwa mujibu wa ripoti ya Daily Record, Carlo Ancelotti atateuliwa kama meneja mpya wa klabu ya Chelsea kabla ya kuanza kwa msimu ujao.

Mimiliki wa klabu ya Chelsea, Roma Abramovich akiwa na Carlo Ancelotti
Ripoti hiyo inadai kwamba mazungumzo na Roman Abramovich yako kwenye hatua za mwisho, na Muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 58 ana karibia kupewa usukani kwa mara nyingine tena.

Awali Carlo Ancelotti alikuwa akihusishwa na kuhamia PSG, lakini ripoti mpya zainadai meneja huyo anakaribia kujiunga na klabu ya Chelsea.

Ripoti ya Ian Gerry katika mtandao wa Daily Record inasema: “Carlo Ancelotti hataelekea PSG kwa sababu atakuwa anarejea London mwezi February. Na pale atakuwa anasubiri muda ufike achukue madaraka ya Antonio Conte katika klabu ya Chelsea. Tayari ameshafanya mazungumzo na klabu hiyo kuhusiana na kurithi nafasi ya Conte, ambaye kila mtu ndani ya klabu anaelewa kwamba hataendelea kusalia katika klabu hiyo baada ya msimu huu.”
Anayetarajiwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Chelsea huyu hapa Anayetarajiwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Chelsea huyu hapa Reviewed by Zero Degree on 12/17/2017 03:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.