Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 31 Decemba, 2017

Nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Gareth bale
Florentino Perez anatarajia kufanya mapinduzi makubwa kwenye kikosi cha klabu ya Real Madrid hata kama itamgharimu kuachana na wachezaji wenye majina makubwa. 

Eden Hazard anaweza kuondoka na mchezaji mwingine kutoka klabu ya Chelsea endapo atajiunga na Real Madrid kwenye majira ya joto. (Don Balon)

Klabu ya Real Madrid inafanya mpango wa kumnasa Harry Kane kwa kumtumia Gareth Bale kama sehemu ya ofa itakayoishawishi Tottenham.

Klabu ya Manchester City inatarajia kumpa ofa ya mkataba mpya beki wake, Nicolas Otamendi.

Chelsea lazima wafanye kila liwezekanalo kuwabakisha Eden Hazard na Thibaut Courtois kikosini - Conte.
 (ESPN)

Klabu ya West Ham ina mpango wa kumsajili aliyekuwa kiungo wa Chelsea Andre Schurrle kutoka Borussia Dortmund. (Bild)

Barcelona itatoa ofa ya pauni milioni 130 kwa ajili ya nyota wa Liverpool, Philippe Coutinho wiki hii.

Manchester United wanatazamia kumrejesha nyumbani Cristiano Ronaldo baada ya nyota huyo kutofautiana na viongozi wa klabu ya Real Madrid.

Jose Mourinho amemwambia 'wakala wake wa siri', Paul Pogba kumsaidia kufanikisha uhamisho wa Paulo Dybala kutoka Juventus.

Alexis Sanchez
Arsene Wenger ana wasiwasi juu ya tofauti iliyopo kati ya Alexis Sanchez na wachezaji wenzake wa Arsenal.

Tottenham wako tayari kuipiku Chelsea kwenye suala la usajili wa kiungo wa Everton, Ross Barkley.

Beki wa Chelsea, Andreas Christensen anafuatiliwa na  klabu ya Barcelona.

Matumaini ya Chelsea na Manchester United kufanikisha uhamisho wa Alex Sandro yameongezeka baada ya klabu ya Juventus kujitokeza mstari wa mbele kutaka kumsajili beki wa Bayer Leverkusen, Wendell Nascimento Borges.

West Ham wana matumaini ya kumtumia Diafra Sakho au Andre Ayew kwenye dili la uhamisho wa Alfie Mawson kutoka Swansea.

Ronald Koeman amemtaja Pep Guardiola kama meneja bora zaidi duniani.

Almamy Toure
Klabu za Watford na Huddersfield ziko kwenye ushindani mkubwa kuwania saini ya beki wa klabu ya Monaco, Almamy Toure ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 12. (Mirror)

Kaka yake na Dele Alli alionekana wakati wa mchezo wa 'El Clasico' kati ya Real Madrid na Barcelona na kuchochea uvumi kwa mashabiki wa Spurs.

Pep Guardiola anajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 50 mwezi Januari kwa ajili ya beki wa klabu ya Barcelona, Samuel Umtiti.

West Ham watatakiwa kulipa kiasi cha pauni milioni 40 kwa ajili ya beki wa kati wa klabu ya Swansea, Alfie Mawson.

Mshambuliaji wa Canada, Cyle Larin anatarajiwa kuachana na uhamisho kwenda Uingereza au Uturuki badala yake ajiunge na Borussia Moenchengladbach.

Liverpool na Everton zinashindania saini ya beki wa klabu ya Preston, Josh Earl.

David Wagner anatarajiwa kufanya usajili mkubwa mwezi Januari kwa kumnasa nyota wa klabu ya Monaco, Terence Kongolo.

Newcastle wako tayari kumuuza Jonjo Shelvey - kama Rafa Benitez atahitaji fedha zaidi.

Joao Mario
Jose Mourinho ana mtaka Joao Mario kutoka Inter Milan wakati Henrikh Mkhitaryan atakapoenda kujiunga na vigogo hao wa Italia.

Manuel Lanzini ni chaguo la kwanza la Liverpool kujaza nafasi ya Philippe Coutinho.

Sean Dyche ana mpango wa kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kumnasa nyota wa klabu ya Nottingham Forest, Joe Worrall. (Sun)

Roy Hodgson amewaonya waliokuwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Uingereza kwamba wataaibika kwenye Kombe la Dunia ncini Urusi. (Telegraph)

Alan Pardew
Meneja wa klabu ya West Brom, Alan Pardew anaamini kwamba Arsene Wenger atatakiwa kuachana na nyota wake, Alexis Sanchez kuelekea mechezo wao dhidi ya Arsenal.

Nyota wa Manchester City, Sergio Aguero ana mpango wa kurejea kwenye klabu yake ya zamani, Independiente ya nchini Argentina.

Manchester United watapokea kiasi cha pauni milioni 1 kutoka Crystal Palace kama watamrejesha Timothy Fosu-Mensah kutoka huko alikokuwa kwa mkopo.

Swansea, Brighton zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili nyota wa Hull City, Jarrod Bowen, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 8.

Glen Johnson yuko kwenye mazungumzo na Stoke City kuhusiana na mkataba mpya miezi sita kabla ya mkataba wake wa sasa kumalizika kwenye majira ya joto. (Daily Mail)

Bayern Munich wamekata tamaa ya kumnasa Jurgen Klopp katika kipindi cha majira ya joto kinachokuja. (Star)

Arsenal wamejitokeza mstari wa mbele kama klabu pekee yenye jitihada za kuweza kufanikisha uhamisho wa beki wa kati kutoka klabu ya Chelsea, David Luiz. (Express)

Leon Britton
Kiungo wa Swansea, Leon Britton ameachana na kazi mpaya kwenye benchi la ufundi la meneja mpya Carlos Carvalhal na badala yake aendelee na kazi yake kama mchezaji kwa kipindi hiki kilichobakia msimu huu.

Jimmy Nicholl atakuwa meneja msaidizi wa klabu ya Rangers wiki ijayo.

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anadai hajui mipango aliyonayo mshambuliaji wake raia wa Chile, Alexis Sanchez kuhusu hatma yake katika klabu hiyo. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 31 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 31 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/31/2017 02:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.