Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 6 Decemba, 2017

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ureno na Klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo
Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Pérez ana mpango wa kuachana na Cristiano Ronaldo na kusajili nyota mwingine atakayechukuwa nafasi ya Mreno huyo.

Andre Gomes amewasilisha ofa katika klabu ya Barcelona inayoweza kupelekea mapinduzi Camp Nou. (Don Balon)

Matumaini ya Chelsea kumsajili Alex Sandro yamechochewa na ripoti zinazodai kwamba Mbrazil huyo anataka kuondoka Juventus.

Meneja wa West Brom, Alan Pardew yuko tayari kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya nyota wa Liverpool, Danny Ings. (Telegraph)

Kwa mujibu wa ripoti za nchini Uhispania, mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata na meneja wake, Antonio Conte wote wanaweza kuhamia Real Madrid katika kipindi cha majira ya joto kichajo.

Klabu ya Everton ilikuwa na matumaini kumsajili beki wa Manchester United, Daley Blind kabla ya kutimuliwa kwa Ronald Koeman.

James Rodriguez 
Muda wa James Rodriguez kukaa na klabu ya Bayern Munich unaweza usiwe mrefu sana, ikiwa Chelsea na Manchester United zinamhitaji mshambuliaji huyo wa nchini Colombia.

Lucas Moura ameitosa ofa ya klabu ya Chelsea na badala yake atajiunga na Beijing Guoan ya China. (Express)

Everton inamchunguza winga wa klabu ya Arsenal, Theo Walcott ikiwa ni mipango ya meneja wa timu hiyo, Sam Allardyce kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji mwezi Januari.

David de Gea amehitaji mshahara unaolingana na ule wa wanaolipwa mishahara mikubwa katika klabu Real Madrid kama ataondoka Manchester United na kurejea Uhispania mwezi Januari au katika kipindi cha majira ya joto mwakani.

Lionel Messi alikataa kusaini mkataba wenye bonasi ya paundi milioni 88 na klabu ya Manchester City ili abaki Barcelona.

Dele Alli ameamua kuachana na kuteua wakala binafsi wakati akiachana na Rob Segal lakini anahusishwa na kampuni ya "The Sports PR Company and Creative Artists Agency".

Meneja wa klabu ya everton, Sam Allardyce
Sam Allardyce hatasafiri na kikosi cha Everton kwenda Cyprus kwenye mechi ya Ligi ya Europa dhidi ya Apollon Limassol kwa sababu ya ratiba yake ya matibabu - Craig Shakespeare ataiongoza timu katika mchezo huo.

Adidas wana ujasiri wa kufanikiwa kukamilisha mkataba wa mamilioni ya fedha na Romelu Lukaku.

Robbie Brady atakuwa nje kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia kwa sababu ya majeraha ya goti.

Mike Ashley ataiuza klabu ya Newcastle United kwa Amanda Staveley na Washirika wa kampuni ya PCP endapo tu watampa ofa ya karibuni paundi milioni 300.

Everton wametangaza kupunguza bei ya vingilio kwa msimu mzima kwa mwaka ujao.

Tim Cahill ametangaza kwamba, ataondoka katika klabu ya Melbourne City haraka iwezekanavyo. (Daily Mail)

Mark Hughes
Mark Hughes anasema kwamba Jese bado ana muda wa kufanya mambo makubwa katika klabu ya Stoke City.

Nyota wa klabu ya Napoli anayewindwa na Manchester City, Faouzi Ghoulam amesaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo ya Serie A.

Valencia wana matumaini ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa klabu ya Everton, Sandro Ramirez mwezi Januari. (Sun)

Manchester United wanaendelea kumfuatili kiungo wa klabu ya Lazio, Sergej Milinkovic-Savic.

Manchester City wana andaa ofa ya paundi milioni 50 kwa ajili ya mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez. 

Krepin Diatta
Chipukizi wa klabu ya Sarpsborg, Krepin Diatta anatazamia kuihama klabu hiyo na amekuwa akiripotiwa kuwa chini ya uangalizi wa maskauti wa Manchester United. (Star)

Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola amekanusha taarifa inayodai klabu hiyo ilimpa Lionel Messi bonasi ya paundi milioni 100 aondoke Barcelona katika kipindi cha majira ya joto kilichopita. (Guardian)

Klabu ya Sevilla inadai kwamba, Steven N'Zonzi hakwenda London siku ya Jumanne kwa ajili ya mazungumzo ya kurejea kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, bali alikwenda kumtembelea mwanaye kwa ruhusa maalum.

Aston Villa wana matumaini ya kumsajili winga wa klabu ya Newcastle, Rolando Aarons kwa bei yenye punguzo kubwa mwezi ujao.

Mark Clattenburg
Mark Clattenburg anasema aliwahi kubadilisha uamuzi wa kuipa Manchester United mpira wa 'golikiki' na badala yake akaipa kona katika mchezo wao mmoja ambao aliuchezesha kwa sababu ya kumwogopa Roy Keane. (Mirror)

Derek McInnes atalazimishwa kujiuzulu nafasi yake katika klabu ya Aberdeen ili afanikishe dili la kurejea Rangers. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 6 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 6 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/06/2017 01:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.