Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 20 Decemba, 2017

Antoine Griezmann
Klabu ya Atletico Madrid iko tayari kumuuza Antoine Griezmann kwenda Man United baada ya kupeleka madai FIFA ikidai mahasimu wao wa La Liga, FC Barcelona walitaka kumsajili nyota huyo kinyume na sheria.

Kibarua cha Benitez kinabaki salama licha ya klabu ya Newcastle kuwa kwenye ukanda wa timu zinazosubiri kushuka daraja katika msimamo wa Ligi Kuu.

Arsenal wanafikiria kutoa ofa ya paundi milioni 42 kumnasa mshambuliaji wa PSV, Hirving Lozano.

Meneja wa Everton, Sam Allardyce atajaribu kumsajili winga wa klabu ya Arsenal, Theo Walcott na pia ana matumaini ya kumpata kiungo wa Sevilla, Steven Nzonzi.

Brighton wanaweza kumsajili Marko Grujic kutoka Liverpool mwezi January baada ya raia huyo wa Serbia kushindwa kupata nafasi ya mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza Anfield.

Klabu ya Nottingham Forest inatarajiwa kuongeza nguvu katika kuwania saini ya golikipa wa Brondby, Frederik Ronnow.

Pape Souare
Klabu ya Marseille ina matamanio ya kumsajili beki wa Crystal Palace, Pape Souare kujaza nafasi ya Patrice Evra. (Mirror)

Jose Mourinho ana fanya mpango wa kuvunja rekodi ya usajili Uingereza kwa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard kwa paundi milioni 90.

Klabu ya Newcastle inamtaka beki wa Chelsea, David Luiz kwa mkopo mwezi ujao.

Brighton wanafanya mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Spartak Moscow na Timu ya Taifa ya Cape Verde, Ze Luis.

Crystal Palace iko mstari wa mbele kutaka kumsajili golikipa wa Manchester United, Sam Johnstone, ambaye yuko Aston Villa kwa mkopo. (Sun)

Paul Clement
Paul Clement yuko hatarini kufukuzwa kazi endapo Swansea itapoteza mechi yao dhidi ya Crystal Palace Jumamosi. (Express)

Nyota wa klabu ya West Ham, Diafra Sakho alianzia benchi kwenye mechi dhidi ya Arsenal baada ya mgogoro na David Moyes kuhusu nafasi yake kikosini na bonasi ta paundi 50,000.

Mechi za Tottenham katika dimba la Wembley zinachelewesha ukarabati wa muhimu katika paa la uwanja wa taifa. (Daily Mail)

Beki wa klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina, Javier Mascherano anakaribia kujiunga na klabu ya Hebei Fortune ya China. (Sport)

Jason Puncheon
Roy Hodgson anaweza kumvua unahodha Jason Puncheon katika klabu ya Crystal Palace kufuatia tukio la kukamatwa na vyombo vya usalama baada ya kuwa amepigana nje ya kumbi za starehe wikendi iliyopita.

Beki wa klabu ya Southampton, Cedric Soares atakosa katika michezo ya kipindi hiki cha sikukuu za Chrismas kwa sababu ya majeraha kwenye paja lake. (Star)

Mashabiki wa klabu ya Manchester United huenda wakalazimika kulipa hadi paundi 133 kwa ajili ya tiketi za kombe la Klabu Bingwa kwenye mchezo wao ugenini dhidi ya Sevilla. (Manchester Evening News)

Chris Coleman
Chris Coleman ataishawishi klabu ya Liverpool imruhusu kiungo wa Wales , Ben Woodburn ajiunge na Sunderland mwezi Januari.

Paul Elliott atakuwa wa kwanza kati ya waliokuwa wachezaji wa ngazi za juu kuingia katika bodi ya FA mwezi ujao. (Times)

Akitegemewa kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu katika klabu Celtic, Marvin Compper amaetajwa kuwa mtu pekee anayeweza kuboresha safu ya ulinzi ya klabu hiyo ya Uskoti. (Record)

Meneja wa Stoke City, Mark Hughes bado anaungwa mkono na bodi ya klabu kabla ya mechi ya Jumamosi dhidi ya West Brom licha ya klabu hiyo kuwa na pointi moja juu ya eneo la kushushwa daraja. (Sky Sports)

Manchester City inapewa nafasi kubwa kushinda mataji manne baada ya kufika nusu fainali ya kombe la Carabao, lakini kwa upande wake meneja wa klabu hiyo, Pep Guardiola anadai ni vigumu sana.

Harry Wilson
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Wales, Harry Wilson amekataa ofa ya mkataba mpya Liverpool na anatarajia kuondoka mwezi ujao. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 20 Decemba, 2017  Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 20 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/20/2017 07:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.