Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 27 Decemba, 2017

Harry Kane
Harry Kane yuko tayari kujiunga na klabu ya Real madrid enapdo rais wa klabu hiyo, Florentino PĂ©rez atamhakikishia kwamba atakuwa mshambuliaji pekee asiyeguswa Bernabeu.

Meneja wa Real Madrid, Zinedene Zidane na rais wa klabu hiyo wamepishana lugha kwenye suala la usajili wa straika mpya - 'Zizou' akisistiza kwamba, Benzema anatosha wakati Florentino Perez akionyesha kuchoshwa na Mfaransa huyo na badala yake anataka kumsajili Kane. (Don Balon)

Southampton wameamua kummuza Virgil van Dijk mwezi Januari - lakini wanahitaji paundi milioni 70 ili kumwachia beki huyo. (Mirror)

Marouane Fellaini anaendeleza msimamo wake wa kutaka alipwe paundi 170,000 kwa wiki akifikiria kuhusu future yake katika klabu ya Manchester United. (Telegraph)

Jack Wilshere
Hatimaye Arsene Wenger ametoa nafasi kwa kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere kupewa mkataba mpya.

Chipukizi wa klabu ya Liverpool, Ben Woodburn anawindwa na Leeds, Norwich, Preston na Sunderland, ambazo zote zinataka kumsajili mshambuliaji huyo kwa mkopo.

Nyota anayewaniwa na Manchester United pamoja na Chelsea, Alex Sandro ameonywa kwamba, anatakiwa alipe fadhila ya imani ambayo klabu ya yake  (Juventus) ilionyesha kwake.

Manchester United wameripotiwa kutangaza dau la paundi milioni 35 kama bei ya Henrikh Mkhitaryan.

Medhi Benatia
Juventus wamekataa ofa ya paundi milioni 35 kutoka Arsenal kwa ajili ya usajili wa Medhi Benatia.

Meneja wa klabu ya West Ham, David Moyes amekiri kuwa na nia ya kumsajili nyota wa Sevilla, Steven N'Zonzi.

Meneja wa Crystal Palace, Roy Hodgson amekiri kufurahishwa na ofa kubwa kwa ajili ya uhamisho wa Wilfried Zaha. (Sun)

Klabu ya Everton imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Besiktas, Cenk Tosun anayekadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 20.

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amekataa kukana ofa ya pauni milioni 53 kwa ajili ya kumnasa kiungo wa Bayern Munich, Arturo Vidal.

Rafa Benitez anaamini ataibadilisha klabu ya Newcastle na kuiweka miongoni mwa klabu nane bora endapo mabadiliko ya umiliki yatafanikiwa. (Daily Mail)

Hirving Lozano
Liverpool na Arsenal zinashindania saini ya mshambuliaji raia wa Mexico, Hirving Lozano ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa paundi milioni 42. (Star)

Barcelona wana majina matano kwenye orodha ya 
wachezaji wanaotegemea kuwasajili kwenye dirisha dogo la mwezi Januari - ambapo miongoni mwa majina hayo ni la kiungo wa klabu ya Arsenal, Mesut Ozil. (Express)

Celtic wanahitaji kiasi cha paundi milioni 20 ili kumwachia mshambuliaji wao, Moussa Dembele.
 (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 27 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 27 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/27/2017 06:09:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.