Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 4 Decemba, 2017

Lionel Messi
Sergi Roberto anasema kwamba, Antonio Conte amemtaka Roman Abramovich ajaribu kumsajili Lionel Messi kuifanya Chelsea iwe na nguvu ya kutetea Taji la Ligi Kuu mbele ya Pep Guardiola na Jose Mourinho. (Don Balon)

Mshambuliaji wa Watford, Troy Deeney ni kinara kwenye orodha ya wachezaji wanaowindwa na meneja wa klabu ya Everton, Sam Allardyce wakati wa uhamisho wa mwezi Januari. (ESPN)

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte
Meneja wa Chelsea, Antonio Conte ameiambia bodi ya klabu hiyo kushugulikia mikataba ya Thibaut Courtois na mchezaji wa safu ya kati Eden Hazard kabla ya Kombe la dunia. (Express)

Everton, West Ham na Swansea wanarajiwa kungangania kumwinda mlinzi wa Augsburg Daniel Opare, 27, in January. (Daily Mail)

Thibaut Courtois anaweza kukataa kusaini mkataba mpya hata kama Chelsea watampa mshahara unaolingana na anaolipwa golikipa wa Manchester United,  David De Gea.

Davinson Sanchez
Tottenham wanazidi kukumbwa na matatizo katika safu yao ya ulinzi kuelekea mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Manchester City baada Davinson Sanchez kutolewa nje kwenye mechi yao dhidi ya Watford.

Mesut Ozil alilisifia benchi la ufundi la Manchester United baada ya Arsenal kuchapwa goli 3-1 na wapinzani wao wa jadi kwenye uwanja wa Emirates Jumamosi. (London Evening Standard)

Pep Guardiola anadai Manchester City lazima waendelee kumfurahisha Raheem Sterling wakitazamia kumpa mkataba mrefu.

Leon Goretzka
Leon Goretzka amesema atafanya maamuzi kuhusiana na mstakabali wa maisha yake katika klabu ya Schalke itakapifika Januari.(Manchester Evening News)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 4 Decemba, 2017  Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 4 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/04/2017 03:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.