Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 18 Decemba, 2017

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo anataka wachezaji wa klabu ya Barcelona waiandalie Real Madrid gwaride la heshima kwenye El Clasico Jumamosi. 

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo anataka mshahara wake uongezwe na kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani ili abaki Real Madrid. (Marca)

Manchester United wanafanya mpango wa kumnasa winga mwenye thamani ya paundi milioni 80 kutoka klabu ya Bordeaux, Malcom.

Mabingwa watetezi wa Sirie A, Juventus pamoja na Real Madrid ni miongoni mwa klabu ambazo zina matamanio makubwa ya kumsajili beki wa Chelsea, David Luiz.


Graham Poll anafikiri kwamba, Dele Alli alitakiwa kutolewa nje kwenye mechi ya Tottenham dhidi ya Manchester City siku ya Jumamosi, iliyomalizika kwa Spurs kuchapwa bao 4-1. (Daily mail)

Klabu ya Newcastle inamtaka mshambuliaji wa RB Salzburg, Dimitri Oberlin mwezi Januari lakini kwa sasa anaichezea FC Basel kwa mkopo.

Kiungo wa klabu ya Swansea na mkufunzi msaidizi, Leon Britton atachukua atachukua nafasi ya meneja wa klabu hiyo, Paul Clement endapo atafukuzwa kazi. (Sun)

Antonio Conte anasema kwamba klabu sita kubwa nyinginezo haziwezi kuruhusu Virgil van Dijk asaini mkataba na Manchester City.

Klabu ya Chelsea iko tayari kumuuza beki wao wa kati kutoka Brazil, David Luiz ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 30.

Arsene Wenger ana amini kwamba, Mesut Ozil ana kiwango cha hali ya juu sana kwa sasa, kitu kinachomfanya astahili kupewa mkataba mpya wenye thamani kubwa.

Manchester United wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya paundi milioni 60 kumnasa beki wa klabu ya Juventus, Alex Sandro mwezi Januari.

Manuel Lanzini 
Nyota wa klabu ya West Ham, Manuel Lanzini yuko hatarini kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kujiangusha kwenye mchezo wao dhidi ya Stoke City, atukio ambalo liko linafanyiwa uchunguzi wa Shirikisho la Soka la Uingereza (FA).

Mauricio Pochettino anasema Dele Alli anahitaji "msaada" baada ya kufanikiwa kukwepa kadi nyekundu katika mechi yao dhidi ya Manchester City.

Chelsea pia iko miongoni mwa vilabu vinyavyowania saini ya mshambuliaji wa Crystal Palace, Wilfried Zaha mwezi Januari. (Mirror)

Christian Benteke anasema hajutii kitendo cha kukosa penati kwenye mechi yao dhidi ya Bournemouth wiki iliyopita. (Star)

Roy Hodgson
Roy Hodgson amelalamikia tuhuma za Eddie Howe kuhusu Wilfried Zaha kujiangusha ili kuipatia Crystal Palace penati.

Liverpool hawatawasilisha ofa kwa ajili ya beki, Virgil van Dijk iwapo klabu ya Southampton haitashusha thamani ya Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka paundi milioni 70. (Independent)

Jose Mourinho ameionya klabu ya Manchester City kwamba ubingwa bado ni wa yeyote, hivyo isifanye sherehe ya kutwaa taji mapema. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 18 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 18 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/18/2017 08:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.