Loading...

Tottenham wanataka kutibua dili la Chelsea kwenye dirisha la usajili mwezi Januari


Kwa mujibu wa 'The Mirror', klabu ya Tottenham iko kwenye mipango ya kutibua dili la Chelsea na kumnasa kiungo wa Everton, Ross Barkley.

Ross Barkley
Katika hali ya kushangaza, Barkley aliachana na uhamisho kwenda Stamford Bridge katika kipindi cha majira ya joto kilichopita na sasa klabu ya Chelsea pamoja na Spurs zote zinajiandaa kutoa ofa mpya kwa ajili ya kumnasa kiungo huyo mwezi januari.

Gazeti la 'The Mirror' la Jumapili limetoa ripoti inayodai kwamba Tottenham iko tayari kutoa ofa kwa ajili ya kumnasa kiungo huyo wakati dirisha la usajili la mwezi januari litakapofunguliwa.

Hata hivyo, kwa mujibu wa 'The Telegraph', Chelsea wana nafasi kubwa ya kuweza kufanikisha uhamisho huo dhidi ya Tottenham kwa sababu wako tayari kufanya mazungumzo muda huu.

Spurs wao wanaona ni bora kusubiri hadi mwisho wa msimu ambapo Barkley atakuwa kama mchezaji huru.

Inasemekana Chelsea na Everton ziko tayari kuhakikisha jambo hilo linakamilika badala ya kuliacha lipitilize mwezi Januari.
Tottenham wanataka kutibua dili la Chelsea kwenye dirisha la usajili mwezi Januari Tottenham wanataka kutibua dili la Chelsea kwenye dirisha la usajili mwezi Januari Reviewed by Zero Degree on 12/31/2017 10:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.