Loading...

Upelelezi wa chanzo cha mauaji ya kimbari Rwanda wakamilika

Rais wa sasa wa Rwanda, Paul Kagame
Majaji wa Ufaransa wamemaliza upelelezi juu ya shambulio la kombora ambalo lilisababisha kuanza kwa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994.

Ofisi ya mwendesha mashitaka sasa wataamua ikiwa waipeleke kesi mbele ya mahakama. 

Majaji wamewalaumu wapiganaji walioongozwa na rais wa sasa wa Rwanda, Paul Kagame kwa kuilenga na kuiangusha ndege iliyokuwa imembeba rais wa wakati huo wa taifa hilo, Juvenal Habyarimana.

Rwanda nayo inailaumu Ufaransa kwa kushiriki kupanga mauaji ya kimbari. Upelelezi umesababisha sintofahamu kati ya mataifa haya mawili, kiasi cha Rwanda kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na ufaransa mwaka 2006, lakini baada ya miaka nane uhusiano huo ulirejeshwa.

Source: BBC Swahili
Upelelezi wa chanzo cha mauaji ya kimbari Rwanda wakamilika Upelelezi wa chanzo cha mauaji ya kimbari Rwanda wakamilika Reviewed by Zero Degree on 12/22/2017 07:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.