Loading...

Video: Manchester United yatolewa nje na Bristol City kwenye michuano ya Carabao


Klabu ya Bristol City, imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Carabao kwa kuwaondosha mabingwa watetezi wa michuano hiyo klabu ya Manchester United.

Bristol walianza kuzifumania nyavu za United kwa goli la Joe Bryan, katika dakika ya 51 ya mchezo. Iliwachukua dakika saba tu kwa Manchester United, kusawazisha goli hilo kupitia kwa Zlatan Ibrahimovic.

 

Shujaa wa Bristol City alikuwa ni kiungo Korey Smith aliyefunga goli la ushindi katika dakika za lala salama.

Kwa upande mwingine, Chelsea walifanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa goli 2-1 dhidi ya AFC Bournemouth.

Kiungo Willian Borges da Silva, ndie aliyeanza kuipatia Chelsea goli la kuongoza katika dakika ya 13 ya mchezo.



Bournemouth wakasawazisha goli hilo katika dakika ya tisini kupitia kwa kiungo Daniel Gosling na mnamo dakika ya 91, mshambuliaji hatari wa Chelsea Alvaro Morata alifunga goli la ushindi lililoipeleka Chelsea nusu fainali.

Michezo ya nusu fainali itapigwa tarehe 9 Januari, 2018 kwa Chelsea kucheza dhidi ya Arsenal na Bristol City kucheza dhidi ya Manchester City.
Video: Manchester United yatolewa nje na Bristol City kwenye michuano ya Carabao Video: Manchester United yatolewa nje na Bristol City kwenye michuano ya Carabao Reviewed by Zero Degree on 12/21/2017 11:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.