Loading...

Zaidi ya asilimia 98 ya wanafunzi wamechaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2018

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo
WANAFUNZI 650,862 (asilimia 98.31), wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2018 kati ya wanafunzi 662,035 waliofaulu.

Vilevile, Serikali imetoa wiki mbili kwa wanafunzi hao kuripoti shule walizopangiwa na kama wakichelewa nafasi zao watapangiwa wanafunzi wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), Selemani Jafo alisema ufaulu huo ni a ongezeko la wanafunzi 124,209 ikiwa ni sawa na asilimia 23.58.

Jafo alisema mwaka huu wanafunzi 1,912 wenye mahitaji maalumu waliofaulu mitihani ya darasa la saba wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwakani.

Alisema wanafunzi 11,173 (asilimia 1.69 ya waliofaulu) hawakupata nafasi ya kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika awamu hiyo ya kwanza ya uchaguzi.

“Sababu iliyosababisha wanafunzi hao kutokuchaguliwa ni uhaba wa miundombinu ya elimu vikiweamo vyumba vya madarasa kwenye baadhi ya halmashauri,” alisema Jafo.

Aliitaja mikoa ambayo halmashauri zake zimeshindwa kuchagua wanafunzi kuwa ni Lindi wanafunzi (170), Mbeya (3,092), Rukwa (4,091), Manyara (1,268), Katavi (976) na Simiyu ( 1,576).

Waziri aliwataka wakuu wa mikoa iliyotajwa kuhakikisha wanafunzi wote wanapata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018.

“Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani wanatakiwa kuripoti shuleni Januari 18, 2018,” alisema Jafo.

Alisema mikoa ambayo ina tatizo la miundombinu ni lazima ikamilishe miundombinu hiyo haraka wanafunzi watakaochaguliwa awamu ya pili waweze kuripoti shuleni kabla ya Februaru 15 mwakani.

Hata hivyo Jafo amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kutumia fursa hiyo vizuri katika kujifunza na kuachana na anasa au starehe ambazo zitawafanya kupata matokeo mabaya kidato cha nne.
Zaidi ya asilimia 98 ya wanafunzi wamechaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2018  Zaidi ya asilimia 98 ya wanafunzi wamechaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2018 Reviewed by Zero Degree on 12/08/2017 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.