Loading...

ACT Wazalendo wapishana na CHADEMA kuhusu uchaguzi jimbo la Kinondoni na Siha

Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Bara, Msafiri Mtemelwa
Wakati zikiwa zimepita siku tatu tangu CHADEMA watangaze kuwa watashiriki uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Kinondoni na Siha leo Chama cha ACT-Wazalendo kimeendelea kushikiria msimamo wao wa kutoshiriki kwenye uchaguzi huo kwa kuwa sababu zilizowafanya wasusie uchaguzi mdogo uliopita, bado hazijafanyiwa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jumapili Januari 21, 2018. Naibu Katibu Mkuu waATC Wazalendo Bara, Msafiri Mtemelwa amesema changamoto walizolalamikia katika uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 13 katika majimbo ya Songea Mjini, Longido na Singida Kaskazini bado hazijafanyiwa kazi.

Mtemelwa amesema bado chama hicho kitaendelea kushinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufanya mageuzi katika mchakato wa uchaguzi.

ACT Wazalendo walilalamikia kuwa kuna matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola dhidi ya vyama vya upinzani kwa lengo la kukisaidia chama tawala CCM.

Majimbo ya Siha na Kindondoni yalikuwa wazi baada ya waliokuwa wabunge wa majimbo hayo kuhamia CCM mwishoni mwa mwaka jana.
ACT Wazalendo wapishana na CHADEMA kuhusu uchaguzi jimbo la Kinondoni na Siha ACT Wazalendo wapishana na CHADEMA kuhusu uchaguzi jimbo la Kinondoni na Siha Reviewed by Zero Degree on 1/21/2018 12:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.