Loading...

Agizo la CCM kwa viongozi wake wa ngazi zote

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, kimewataka viongozi wake wa ngazi zote kuisimamia serikali katika ngazi zote na kuhakikisha wanajishughulisha na kutatua shida za wananchi kwenye maeneo yao.

Polepole ameeleza hayo katika kikao kilichokuwa na lengo la kuimarisha na kukijenga chama hicho kilichofanyika Mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Moshi mjini huku kikiongozwa na mwenyekiti wa wilaya Alhaji Shamba na kuhudhuriwa na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Peter Patrick Boisafi, Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Kippi Warioba, wazee mashuhuri, viongozi wa dini pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu za Kata.

"Mwaka huu ni wa ujenzi wa chama, kukumbushana misingi ya CCM, kutazama madhaifu na umadhubuti wake katika maeneo yote. Wanachama na viongozi muelewe Katiba, kanuni, taratibu na miongozo ya chama na zaidi viongozi msikilize watu na mtatue shida zao. Kiongozi wa CCM soma na somo kubwa kabisa lipo kwa watu, kuwasikiliza, kuelewa shida zao na malalamiko yao, hakuna somo zuri kama hilo kutoka kwa watu", alisema Humphrey Polepole.

Kwa upande mwingine, Polepole amewasisitiza wajumbe walioweza kuhudhuria kikao hicho dhana ya CCM ambayo ni kuisimamia serikali katika kila nyanja.
Agizo la CCM kwa viongozi wake wa ngazi zote Agizo la CCM kwa viongozi wake wa ngazi zote Reviewed by Zero Degree on 1/20/2018 07:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.