Loading...

Anayepewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Coutinho Liverpool


Baada ya Philippe Coutinho kwenda Barcelona, klabu ya Liverpool sasa iko mawindoni kutafuta mtu sahihi wa kurithi nafasi ya Mbrazil huyo.


Leon Goretzka
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Jurgen Klopp anataka kujaza nafasi ya Mbrazil huyo mwezi huu na tayari ameshataja watu kadhaa anaohisi wanafaa. Lakini kwa sasa amemfanya kiungo wa Schalke 04, Leon Goretzka kuwa chaguo lake la kwanza.

Wiki iliyopita kuna ripoti zilitolewa zikidai kwamba, klabu ya Bayern Munich inakaribia kufikia makubaliano na nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 na anatarajiwa kujiunga na Mabingwa watetezi wa Ligi ya Bundesliga akiwa kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika mwisho wa msimu huu.

Hata hivyo, klabu ya Liverpool ina mawasiliano naye na inaweza kumshawishi nyota huyo ahamie Anfield.

Liverpool pia wamekuwa wakihusishwa na kuwania saini ya Thomas Lemar, lakini inaonekana hawatapoteza muda kuhangaikia saini ya nyota huyo wa Monaco.

Wekundu hao walijaribu kumsajili nyota huyo kwenye majira ya joto lakini klabu ya Monaco ilkataa ofa yao. Mabingwa hao wa Ligue 1 pia walisema hawako tayari kumruhusu aondoke mwezi Januari.

 Kevin Strootman
Wakati huo huo, Liverpool pia wanahusishwa na kuwania saini ya kiungo wa Roma, Kevin Strootman.
Anayepewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Coutinho Liverpool Anayepewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Coutinho Liverpool Reviewed by Zero Degree on 1/10/2018 02:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.