Loading...

Arsenal, Chelsea kushindania saini ya beki huyu


Ikiwa ni mipango ya kuimarisha safu ya ulinzi, Arsenal na Chelsea zinamfuatilia beki wa klabu ya Burnley, James Tarkowski kwenye dirisha la usajili Januari hii.

Kwa mujibu wa taarifa ya 'Daily Star', klabu hizo zilikuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya Virgil Van Dijk, lakini uhamisho wake kuelekea Liverpool uliovunja rekodi umezilazimisha zitazame kwingine, na nyota huyo wa klabu ya Burnley anaonekana kuwa chagua pekee.

James Tarkowski
Thamani yake imeongezeka akiwa Burnley: Alinunuliwa kwa pauni milioni 3.6 mwanzoni mwa mwaka 2017, lakini kwa sasa anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 30: Uhamisho huo unaweza kuisaidia klabu kukuza kipato.

Wakati Arsene Wenger akiwa na Tarkowski kwenye mipango yake, anafikiria pia kuwasajili Jonny Evans au David Luiz.

Ukiziacha Chelsea na Arsenal, vinara wa EPL, Manchester City pia wanamfuatilia beki huyo kutoka klabu ya Burnley, ambayo iko nafasi ya 7 kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Arsenal, Chelsea kushindania saini ya beki huyu Arsenal, Chelsea kushindania saini ya beki huyu Reviewed by Zero Degree on 1/01/2018 06:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.