Loading...

Baada ya kufeli kwa Sanchez, Guardiola ageukia kwa nyota huyu wa Liverpool


Emre Can anaweza kuondoka Liverpool kama mchezaji huru, wakati mkataba wake wa sasa utakapoisha mwishoni mwa msimu huu.

Can amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda kujiunga na Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A), Juventus. Mkataba wa mjerumani huo na klabu ya Liverpool unalizika mwishoni mwa msimu huu. Hali hiyo inapelekea uwepo wa uvumi mkubwa kuhusu 'future' yake.

Taarifa ya tovuti moja ya nchini Uingereza inadai Manchester City wamejitokeza kuitaka saini ya kiungo huyo waLiverpool, Emre Can.

Siku chache zilizopita Can alizungumzia kuhusiana na tetesi zilizoenea kuhusu uhamisho wake, akisisitiza kwamba bado hajafanya maamuzi yoyote juu ya klabu anayotaka kuichezea baada ya mkataba wake kumalizika.

Kiungo wa klabu ya Liverpool na Timu ya Taifa ya Ujerumani, Emre Can
Kwa mujibu wa taarifa ya tovuti hiyo, Can alisema: “Wakala wangu anashughulikia kila kitu lakini nitakuwepo hapa hadi kwenye majira ya joto.”

“Sijasaini chochote na Juventus au yeyote. Nazungumza na kila mtu. Bila shaka, nazungumza na Liverpool. Kwanini isiwe hivyo? Bado nina mkataba hapa. Hii ni klabu nzuri.

“Sina cha kusema, wakala wangu ndiye anayefanya kila kitu. Mimi niko makini kuona matukio yanavyokwenda, maendeleo ya kiwango changu na mchezo kwa ujumla. Nitajitoa kwa kila kitu katika timu hii.”
Baada ya kufeli kwa Sanchez, Guardiola ageukia kwa nyota huyu wa Liverpool Baada ya kufeli kwa Sanchez, Guardiola ageukia kwa nyota huyu wa Liverpool Reviewed by Zero Degree on 1/20/2018 10:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.