Loading...

Baada ya kusaini mkataba mpya Manchester United, Mourinho aizodoa Chelsea


Jose Mourinho amedai kwamba mkataba wake mpya katika klabu ya Manchester United ni wa pekee zaidi kuliko mkataba wowote ule aliosaini akiwa Chelsea au Real Madrid.


Mreno huyo alijiunga na mashetani wekundu mwaka 2016 na kuingoza klabu hiyo hadi Ligi ya Mabingwa kwa kushinda taji la ligi ya Europa.

Manchester United pia ilishinda taji la michuano ya Carabao na licha ya kuwa nyuma ya vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza, Manchester City kwa jumla ya pointi 12, klabu hiyo imempa mkataba mpya Mreno huyo, mkataba ambao anaukubali sana kuliko mikataba yake yote iliyopita.
"Ni mkataba wa pekee kwangu kwa sababu siku zote nimekuwa nikipewa mikataba mipya na klabu baada ya kupata mafanikio makubwa," Mourinho aliiambia MUTV. "Bila shaka nina furaha kufanya hivyo. Lakini inaonyesha ni hali ya uaminifu, uelewa, na imani ya kazi ndio imepelekea kupata mafaniko hayo makubwa.

"Nilisaini mkataba mpya katika klabu ya Chelsea, baada ya kutwaa Taji la Ligi Kuu, Inter Milan, baada ya kutwaa ngao ya hisani, na Real Madrid baada ya kutwaa Taji la La Liga. Hapa ni matokeo ya kazi yangu tu.

"Tunaminiana, tunafurahiana. Ninafanya vitu ambavyo mmiliki pamoja na bodi ya klabu wanatambua ni sahihi kwa faida ya baadae.

"Wananionyesha tamaa waliyonayo, wanatimiza ahadi zao, na wanahamu ya kwenda katika ueleko sahihi.

"Juu ya yote, uhusiano wangu na wachezaji ni nzuri sana. Nina furahia kusaini mkataba mpya na kujikita katika klabu ambayo ninafanya kazi yangu kwa amani na furaha kubwa."
Baada ya kusaini mkataba mpya Manchester United, Mourinho aizodoa Chelsea Baada ya kusaini mkataba mpya Manchester United, Mourinho aizodoa Chelsea Reviewed by Zero Degree on 1/26/2018 07:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.