Loading...

Borussia Dortmund yaikana klabu ya Arsenal

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Gabon na klabu ya Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang
Meneja wa Borussia Dortmund, Peter Stoger anasema kuwa klabu yake bado haijapokea ombi la kumsajili Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Arsenal.

Mshambuliaji huyo wa Timu ya Taifa ya Gabon ambaye anawindwa na 'The Gunners, hakujumuishwa katika kikosi kilichosafiri kwenda kwenye mechi ya klabu hiyo dhidi ya Hertha berlin siku ya Ijumaa ambayo ililisha kwa timu hizo kutoka sare ya goli 1-1.

Meneja wa klabu ya Borussia Dortmund, Peter Stoger
"Hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kuhusu uhamisho wa Aubameyang, yote yanayoendelea ni uvumi tu," alisema Stoger.

"Tunafanya mpango pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang kuona namna atakavyorejea kwenye kikosi cha kwanza cha timu."

Aubameyang pia alikosa mechi ya Jumapili iliyoisha kwa sare ya 0-0 dhidi ya Wolfsburg baada ya kushindwa kuhudhuria mkutano wa timu.

Mchezaji huyo mwenye urmi wa miaka 28 ni mshambuliai wa Dortmund mwenye magoli mengi msimu huu akiwa na mabao13 katika mechi 15 alizoichezea timu yake.
Borussia Dortmund yaikana klabu ya Arsenal Borussia Dortmund yaikana klabu ya Arsenal Reviewed by Zero Degree on 1/20/2018 07:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.