Loading...

Chelsea yashauriwa kumsajili nyota huyu kutoka Arsenal

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte
Chelsea iko sokoni kwenye mawindo ya nguvu mpya katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Klabu hiyo imekuwa ikuwafuatilia nyota ka, Andy Carroll na Peter Crouch, huku jina jipya lililoongezeka kwenye orodha yao likiwa ni la Edin Dzeko. 

Hata hivyo, aliyekuwa nyota wa Uingereza, Ray Parlour anasisitiza kwamba Chelsea inatakiwa iachane na Carroll na badala yake imsajili mshambuliaji wa  Arsenal, Olivier Giroud kwa sababu ana amini nyota huyo aatakuwa suluhisho la matatizo katika safu ya ushambuliaji kwenye kikosi cha Antonio Conte.

Mshambuliaji wa Klabu ya Arsenal, Oliver Giroud
Akizungumza na Sky Sports, kiungo huyo wa zamani wa Arsenal, Ray Parlour kwa pande alisema, ana amini kwamba Conte anatakiwa aelekeze nguvu zake kwenye mchakato wa uhamisho wa Giroud na wakati huo huo anahisi Arsene Wenger hatakuwa tayari kumuuza nyota huyo kwenda Chelsea, lakini ana uhakika mshambuliaji huyo wa Ufaransa atakuwa tayari kuelekea Stamford Bridge. 

“Atawafaa sana”, Parlour aliiambia Sky Sports na kuongeza:

“Kama Arsenal watataka kumwacha mchezaji wao mwingine ajiunge na maadui zao, hilo ni suala jingine.

“Lakini naina uhakika Chelsea wakitoa ofa ya kawaida, mchezaji huyo anaweza kushawishika kwa uhamisho huo kwani hatahitaji kwenda kuanza maisha mapya sehemu nyingine, na kujikuta anabaki London kama ilivyokuwa kwa Petr Cech, aliyekuwa ameishi kwa muda mrefu katika mji wa London na kutaka abaki pale pale.”
Chelsea yashauriwa kumsajili nyota huyu kutoka Arsenal Chelsea yashauriwa kumsajili nyota huyu kutoka Arsenal Reviewed by Zero Degree on 1/19/2018 08:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.