Loading...

DC aleza sababu ya kuwakamata wanafunzi waliopata ujauzito


Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara Sebastian Waryuba, ametoa ufafanuzi kuhusu suala lililoleta sintofahamu kwa jamii, la kuwakamata mabinti wanafunzi waliopata ujauzito na kuwapeleka polisi.

Kwa mujibu wa taarifa ya EATV, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa amefikia uamuzi huo ili kuweza kuisaidia serikali kubaini watu waliosababisha kukatisha masomo kwa mabinti hao, ambao mara nyingi wamekuwa wakihofia kuwataja.

Mheshimiwa Waryuba amesema kuwa mabinti hao pamoja na wazazi wao wametoa ushirikiano wa kutosha kwa serikali kwa kuwataja, huku wakionyesha kujutia baada ya kufikishwa polisi, lakini wote waliachwa huru baada ya kukamilisha mahojiano.

Habari zaidi bofya hapo chini:
DC aleza sababu ya kuwakamata wanafunzi waliopata ujauzito DC aleza sababu ya kuwakamata wanafunzi waliopata ujauzito Reviewed by Zero Degree on 1/09/2018 09:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.