Loading...

Dortmund imetoa taarifa rasmi kuhusu suala la uhamisho wa Aubameyang

Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang
Klabu ya Borussia Dortmund imetoa taarifa rasmi kuhusu 'future' ya Pierre-Emerick Aubameyang, huku kukiwa na uvumi kwamba nyota huyo anaenda Arsenal mwezi huu.

Inafahamika kuwa 'The Gunners' wamejaribu kutoa ofa zaidi ya mara moja ili kumnasa Aubameyang, lakini ofa zote hazikufikia kiasi cha pauni milioni 61 ambacho Dortmund inahitaji ili kumwachia raia huyo wa Gabon.

Kuelekea mechi ya Dortmund na Freiburg, mkurugenzi wa kandanda wa Michael Zorc alisema: “Tumejiandaa kutekeleza uhamisho chini ya vigezo flani - lakini tu kama vigezo hivi vitatimizwa. Arsenal imefanya majaribio kadhaa hadi sasa.

“Tumekataa ofa zote hadi sasa. Aidha mahitaji yetu yatatimizwa, basi kunaweza kuwa na uhamisho mwingine au vinginevyo hakifanyika kitu chochote na Auba ataendelea kuichezea Dortmund hadi kwenye majira ya joto. Suala hilo pia limejadiliwa na kukubaliwa na familia ya Aubameyang.”
Dortmund imetoa taarifa rasmi kuhusu suala la uhamisho wa Aubameyang Dortmund imetoa taarifa rasmi kuhusu suala la uhamisho wa Aubameyang Reviewed by Zero Degree on 1/29/2018 10:17:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.