Loading...

Gary Neville amemtaka Mourinho atibue dili jingine la Manchester City

Gary Neville
Shujaa wa Manchester United, Gary Neville ana amini kuwa klabu yake ya zamani inatakiwa ishindane na Manchester City kuwania saini ya Aymeric Laporte.

Ripoti mbali mbali zimekuwa zikiihusisha klabu ya Manchester City na uhamisho Laporte tangu kuwasili kwa Pep Guardiola na inaonekana mkufunzi huyo yuko kwenye hatua nzuri kumnasa beki huyo wa Athletic Bilbao.

 Aymeric Laporte
Kwa upande wake, Gary Neville anafahamu vizuri juu ya uwezo mkubwa wa Laporte tangu alipokuwa kama mkufunzi wa klabu ya Valencia na amemtaka Jose Mourinho atibue dili la uhamisho la Manchester City kwa kumnasa beki huyo raia wa Ufaransa.

“Katika kipindi changa kifupi kwenye ligi ya Uhispania tulicheza nao mara tatu! Kijana huyu anaweza kucheza kwa kweli! Manchester United inatakiwa imsajili,’’ aliandika beki huyo wa zamani wa Manchester united.

“Ni vigumu sana kupata wachezaji kutoka Bilbao na ni gharama sana lakini kijana huyo ni mchezaji mzuri sana.”
Gary Neville amemtaka Mourinho atibue dili jingine la Manchester City Gary Neville amemtaka Mourinho atibue dili jingine la Manchester City Reviewed by Zero Degree on 1/25/2018 12:59:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.