Loading...

Hatimaye klabu ya Arsenal imekubali kulipa ada ya uhamisho wa Aubameyang

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang
Klabu ya Arsenal imekubali kuilipa Borussia Dortmund dau la paundi milioni 60 ili kumnasa straika wao, Pierre-Emerick Aubameyang dili ambalo linavunja rekodi ya klabu hiyo kwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa kiwango kikubwa cha fedha.

Awali 'The Gunners' walitoa ofa ya pauni milioni 50 ambayo ilikataliwa na klabu hiyo, huku mkurugenzi wa michezo wa Dortmund, Michael Zorc akisema kuwa watamruhusu nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 aondoke kama mahitaji yao yatatimizwa.

Arsenal imempatia, Aubameyang mkataba wa miaka mitatu na nusu ambao atakuwa akilipwa paundi 180,000 kwa wiki wakati timu hiyo ikiwa katika harakati za kuimarisha eneo lake la ushambuliaji.

Dortmund ilihitaji kumsajili Giroud laki uhamisho wa Mfaransa huyo ulikwama baada ya kufuatia familia yake kumuhitaji kusalia England.

Kutua kwa Aubameyang ndani ya Arsenal kunatoa nafasi kwa Giroud kuelekea Chelsea kwa dau la paundi milioni 35 kufuatia mazungumzo yaliyofanywa wiki iliyopita.
Hatimaye klabu ya Arsenal imekubali kulipa ada ya uhamisho wa Aubameyang Hatimaye klabu ya Arsenal imekubali kulipa ada ya uhamisho wa Aubameyang Reviewed by Zero Degree on 1/30/2018 09:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.