Loading...

Jupp Heynckes azungumzia 'future' ya Arturo Vidal

Arturo Vidal 
Arturo Vidal amekuwa akihusishwa na kuondoka Alinnaz Arena, huku Anotino Conte akonekana kuwa na matamanio makubwa ya kumnasa kiungo huyo.

Iliaminika kwamba Chelsea walitoa ofa ya pauni milioni 33 kwa ajili ya kumsajili raia huyo wa Chile kutoka Bayern Munich mwezi huu.

Siku chache zilizopita, Conte alisema, “Daima ningependelea Vidal awe na mimi.”

Jupp Heynckes
Hata hivyo, Jupp Heynckes amesema kwamba hakuna ofa yoyote ambayo klabu ya Bayer Munich imekwishapokea kwa ajili ya usajili wa Vidal hadi hivi sasa. Pia amekanusha kuwepo kwa uwezekano wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 kuondoka mwezi huu.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumamosi hii, Heynckes alisema, “Hakuna mawasiliano kati ya Chelsea na Bayern Munich.”

“Hatutamuuza Arturo Vidal au mchezaji mwingine yeyeto mwezi huu.
Jupp Heynckes azungumzia 'future' ya Arturo Vidal Jupp Heynckes azungumzia 'future' ya Arturo Vidal Reviewed by Zero Degree on 1/06/2018 08:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.