Loading...

Kampuni ya Dangote yaagizwa kulipa wachimba wa madini ya jasi kwa wakati


KAMPUNI ya Saruji ya Dangote imetakiwa kuwalipa kwa wakati wachimbaji wa madini ya jasi ili kuwawezesha kulipa kodi zao kwa serikali kulingana na taratibu zilizopo.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa kauli hiyo juzi alipotembelea kiwandani hapo wakati wa ziara yake ya kutembelea mikoa ya Lindi na Mtwara. Naibu Waziri amesema pia ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kuandaa rasimu ya mkataba utakaowezesha wachimbaji wadogo wa madini ya jasi kutatua changamoto zilizopo baina yao na kiwanda husika.

“Andaeni rasimu ya mkataba ili kila mmoja auze madini yake kwa bei inayoeleweka bila kuoneana na kila mmoja apate faida anayostahili,” alisema Biteko.

Kwa upande wake, Mkurugezi Mtendaji wa Mitambo ya Uzalishaji katika Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha alisema kulikuwepo na tatizo la malipo isipokuwa hivi sasa tatizo limeshughulikiwa, na kuahidi kuwa wachimbaji wa madini watalipwa kwa wakati.

Raithatha aliongeza kuwa kiwanda hicho kipo tayari kufanya kazi na wachimbaji wa jasi kwa kuwa malighafi nyingi za kutengeneza saruji zinatoka kwa wachimbaji hao jambo linaloimarisha uhusiano kati ya pande husika. Aidha, ameishukuru serikali kwa uhusiano mzuri kati yake na kiwanda hicho na pia amemshukuru Naibu Waziri kwa kuwatembel
Kampuni ya Dangote yaagizwa kulipa wachimba wa madini ya jasi kwa wakati Kampuni ya Dangote yaagizwa kulipa wachimba wa madini ya jasi kwa wakati Reviewed by Zero Degree on 1/21/2018 05:54:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.