Je, Sanchez, Mkhitaryan na Aubameyang watakuwa na haki ya kushiriki michuano ya Ulaya?
Henrikh Mkhitaryan pia atakuwa na haki ya kushiriki Ligi ya Europa akiwa na kikosi cha Arsenal kama dili la kujiunga na klabu hiyo litakamilika.
Wakati huo huo, Arsenal wameulizia pia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Aubameyang, kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo ya Bundesliga. Hata hivyo, kama nyota huyo atafanikiwa kujiunga na klabu ya Arsenal kwenye dirisha hili la usajili, hatakuwa na haki ya kushiriki Ligi ya Europa akiwa na klabu hiyo ya Uingereza.
Licha ya kwamba Sanchez alishacheza Ligi ya Europa akiwa na Arsenal msimu huu, sheria inamruhusu Sanchez kucheza Ligi ya Mabingwa akiwa Manchester United kwa sababu ni michuano tofauti na ambayo 'The Gunners' inashiriki.
Sheria hiyo hiyo, inampa haki Mkhitaryan kushiriki Ligi ya Europa akiwa na Arsenal, licha ya kuichezea Manchester United kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Kanuni za UEFA zinasema kwamba, mchezaji mpya haruhusiwa kushiriki michuano ya ulaya kama alishiriki michuano hiyo akiwa na klabu nyingine, au aliichezea klabu ambayo kwa wakati huo nayo iko kwenye michuano sawa na klabu yake mpya.
Pierre-Emerick Aubameyang |
Hii inamaana kwamba, suala la Borussia Dortmund kwenda kushiriki Ligi ya Europa baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa nyuma ya klabu ya Tottenham na Real Madrid linamkosesha Aubameyang haki ya kushiriki Ligi ya Europa katika klabu yoyote msimu huu, licha ya kwamba mechi yao ya kwanza katika ligi hiyo itachezwa mwezi ujao.
Je, Sanchez, Mkhitaryan na Aubameyang watakuwa na haki ya kushiriki michuano ya Ulaya?
Reviewed by Zero Degree
on
1/21/2018 05:23:00 PM
Rating: